
Animal health Professional @drama @watching movies #Biologist_Mathematician. Modern science of genetics
west midland
Joined June 2023
- Tweets18.7K
- Following2.7K
- Followers1.4K
- Likes14.3K
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
โUwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.โ
Yoshua 1:9
๐๐ผ
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 502
Mhe. Lissu anaendelea
Anasema uamuzi huu wa kunikuta na hatia na kosa ambalo sikushtakiwa nalo, sikujitetea ni kosa la kutengeneza, effect yake ni kwamba unatoa kinga ya kisiasa kwa wale ambao walihusika mauaji amkubwa ya kisiasa, watatoka na kusema wauaji walishapataikana.
Serikali ya Samia imeua watu wengi zaidi ukiachilia historia ya vita vya majimaji, hawa mass murderers watashangilia sana na uamuzi huu kwasababu mmewapa sababu ya kusema aliyesababisha mauaji ya Oktoba 2025 amepatikana na hatia lakini hii haitafunika ukweli.
Serikali ya Mwalimu Nyerere iliuwa watu 37 mwaka 1977 na iliwajibika, Peter Kisumo alikuwa Mkuu wa Mkoa w Shinyanga alijiuzulu, na wengine akiwemo Mwinyi.
Leo watu 518 walioripotiwa kwa uchache hakuna aliyewajibishwa, uamuzi wenu hautaficha hiyo kashfa.
Kwenye sentences guidelines za Mahakama hii, inasema lazima adhabu ya faini itolewe isipokuwa kama ni grave offence, kosa nililoshtakiwa nalo sio grave.
Waheshimiwa Majaji hukumu mnayo, ambayo mmeagizwa muitoe, itoeni nawashukuruni sana.
Jaji Ndunguru anawasha mic anasema tumesikiliza hoja za pande zote na katika kutoa adhabu tumezingatia sababu kadha wa kadha.
Kwanza mshtakiwa umeomba dhamana ili ukate rufaa, tumeangalia hoja ya ugonjwa na kuwa wewe ni mkosaji wa kwanza, hoja ya adhabu ya faini au kifungo.
Kifungu cha 390 hakijatoa adhabu na ukisoma kanuni ya adhabu kifungu cha 35 kinahusika pale ambapo hakuna adhabu.
Adhabu ni kifungo kisichozidi miaka 5 au fani au vyote viwili na hakijaelekeza faini ni kiasi gani.
Tunajua kuwa pale ambapo fani na kifungo vinakuwa vinatolewa first option ni faini.
Tumesoma na maamuzi mbalimbali na mengine ambayo tumeshayasema mfano kuzuia uchaguzi ni kukiuka katiba, ukisoma Ibara ya 30(1) imeeleza kuwa hutakiwa kuingilia haki za mtu mwingine.
Mahakama inatoa adhabu kwa mshitakiwa kutumikia kifungo cha muda wa miaka 4 na una haki ya kukata rufaa.
Majaji wanatoka.
Naomba Repost yako.
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Finally some light at the end of the tunnelโบ๏ธโค๏ธ๐
@GeoConstructors @GeoConstructors @GeoConstructors
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 500
Mhe. Lissu amemaliza kuteta jambo na Mawakili wake, Mawakili wanarudi kwenye nafasi zao.
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nashukuru kwa nafasi, naomba mnisikilize kwa umakini na muandike kwa umakini.
Leo ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kuitwa Mhaini, kosa ambalo kwa katiba ya nchi yetu ndio kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndio kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, adhabu yake inaweza kuwa kifo baada ya siku 577 za hilo wingu jeusi la adhabu ya kifo kuningโingโinia juu ya kichwa changu, mmeniita mchochezi kosa ambalo halijapangiwa adhabu.
Mmeniita mchochezi na Wakili wa Serikali Mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini????
Maana yake ni nini waheshimiwa majaji?
Kosa nililoshtakiwa nalo halikuwa kosa na nyie wenyewe mmesema halikuwa kosa, kwahiyo nilikaa siku 577 Gereza la Ukonga bila kosa lolote.
Waheshimiwa majaji kauli yenu kwamba halikuwa kosa mmekubaliana na msimamo wangu na ushahidi wangu.
Kuna kitu kimoja hamjakisema na nitakisema for the record na ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa ni kesi ya kisiasa tuu, kugeuza Mahakama ya jinai kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa.
Kwa hukumu yenu ya leo mmethibitisha hilo, ni Political persecution, hivyo inabidi visababu vitengenezwa vya kumfunga huyu mpinzani wao wa kisiasa na visababu vyenyewe ni kosa la uchochezi ambalo nyie Majaji mmelitengeneza, sikushtakiwa kwa uchochezi, nilishtakiwa nje ya uhaini.
Nilishtakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo, mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, with all due respect mmefanya hivi kwasababu ya maelekezo ya kisiasa, hana kosa ila asiachiwe hivi hivi ataonekana ameshinda, Serikali itaaibika, anayetupa Ujaji ataaibika, ndivyo mlivyofanya leo.
Ninajua mnahukumu, ninajua, I feel it in my heart kwa bahati mbaya sana mmefanya kile ambacho Mahakama kuu ya Kenya ilikifanya mwaka 1954 kwenye kesi ya Jomo Kenyatta.
Mahakama Kuu ya Kenya ilimpata na hatia Mzee Kenyatta ingawa historia ilikuwa inajua kuwa hamna kosa lolote, ndicho ambacho mmefanya leo Waheshimiwa majaji.
Historia haijawa na wema sana kwa Majaji ambao wamegeuza Mahakama zao kuwa mahali pakuadhibia wasiokuwa na hatia ili kuwaridhisha walioko madarakani kwasababu mnaadhibu mtu ambaye mnajua hana hatia na Dunia inajua hana hatia.
Waheshimiwa Majaji Wasiokuwa na hatia kama mimi huwa hawaombi msamaha, unaomba msamaha kama una hatia au kama umekosa.
Huombi msamaha unapokuwa huna hatia, nataka niwe very clear kuwa haya nitakayoyasema yasichukuliwe kuwa naomba msamaha, I am completely innocent lakin kwa vile Wakili mkuu wa Serikali amezungumza naomba nimjibu,
Kwanza kabisa, amesema kwenye kifungu cha 35 ambacho amekiombea adhabu kali amesema adhabu ya juu ni kifungo cha miaka 5 au faini au vyote viwili.
Sheria inapotoa adhabu ya aina hiyo faini au kifungo, Mahakama inatakiwa ifanye nini? katika kesi ya Salum Shaban vs R (1985) TLR 71 ambapo Mahakama hii ilisema pale ambapo Bunge limetoa option ya faini au kifungo, Mahakama lazima itoe kwanza adhabu ya faini kwanza.
Kwahiyo mnapotafakari adhabu kali iliyoombwa na Wakili Mkuu wa Serikali msije mkasahau msimamo huu wa kisheria ikiwemo kesi ya Alice Nyawira Ndungu vs R Criminal Appeal No 40 of 2022, Elias Ndikumana vs R Criminal Appeal No 39 of 2022 na mashauri mengine mengi ambayo nina uhakika mnayafaham.
Kuna maneno yamezungumzwa hapa na Wakili Mkuu wa Serikali, amejigeuza kuwa shahidi, amesema kwamba haya makosa ya uchochezi yamekuwa ni makosa mengi sana kwa mujibu wa taarifa za polisi, na kwa mujibu wa hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman.
Part 501 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
"Mkamzike Mzee Alute Lissu Mughwai" Mhe. @TunduALissu akitoka mahakamani baada ya kuhukumiwa miaka 4 Jela.
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
#TajiriLaKihaya
TUNDU LISSU NI MMOJA TU!
* Historia haijawa na wema sana kwa Majaji ambao wamegeuza Mahakama zao kuwa mahali pakuadhibia wasiokuwa na hatia ili kuwaridhisha walioko madarakani kwasababu mnaadhibu mtu ambaye mnajua hana hatia na Dunia inajua hana hatia.
Waheshimiwa Majaji Wasiokuwa na hatia kama mimi huwa hawaombi msamaha, unaomba msamaha kama una hatia au kama umekosa.
Huombi msamaha unapokuwa huna hatia, nataka niwe very clear kuwa haya nitakayoyasema yasichukuliwe kuwa naomba msamaha, I am completely innocent lakin kwa vile Wakili mkuu wa Serikali amezungumza naomba nimjibu, *
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Can confirm: we love each other so much as TanzaniansโSisi ni ndugu. The love Tundu Lissu has received from our compatriots and colleagues beyond our borders is unmatched. May we fix our country and live freely as Mwalimu left us.
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Lissu kajitetea mwenyewe kwenye kesi ambayo hukumu yake ni kunyongwa. A man with balls indeed.
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Imagine unamhukumu kifungo cha miaka minne mzee wa miaka 58, aliyepigwa risasi 16, akapitia zaidi ya upasuaji 20, mkamfutia ubunge wake akiwa bado anapatiwa matibabu nje ya nchi
Mkamnyima gharama za matibabu, Leo kosa lake ni kudai mabadiliko, haki na utawala bora katika nchi yake mnamuona muovu?
Amekaa siku 577 gerezani kwa kesi uhaini. Leo mmeshindwa kuthibitisha uhaini wake mnabadilisha kibao mnamhukumu kwa uchochezi? Hii ni historia ambayo haitasahaulika๐ญ๐
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Mtu mmoja tu anaamua kuzima internet nchi nzima!!
Utawala wa aina hii ndio tunaukataa na kuupinga.
Nchi haiwezi kuendeshwa kwa mood na hisia za mtu mmoja.
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Since Oct 29, 2025 Iโve stepped away from politics to spend a few months in the UAE. But politics is a lifestyle; it affects us all.
Iโm disgusted by the lives lost. A family friend disappeared that day. ๐
I stand with Tundu Lissu and hope heโs freed soon.
#FreeTunduLissu
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Wakati Lissu anafanya mitigation alianza kwa kusema;
โHistoria haijawahi kuwa nzuri kwa Majaji wanaowaonea wasio na hatiaโ
na akamaliza kwa kusema โMimi siombi msamaha kwa kuwa sio mkosaji, kwa sasa nimemaliza, toeni huo uamuzi mlioelekezwaโ ๐ช๐ฟ๐ช๐ฟ๐ช๐ฟ
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
โSheria inapotaja adhabu ya faini au kifungo, ni lazima kwanza itoe adhabu ya faini. Huu ni msimamo wa kisheria.โ
โMkinipa maximum sentence itakuwa ni ushaidi kuwa mmeelekezwa.โ
Soma kwa sauti ya LISSU ndio utapata vibe๐
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
โWaheshimiwa Majaji, kwa bahati mbaya sana, mmefanya kile ambacho Mahakama Kuu ya Kenya ilifanya mwaka 1954 katika kesi ya Mzee Jomo Kenyatta. Walimuadhibu kwa sababu ya kuwa mpinzani wa wakoloni. Historia haijawahi kuwaacha salama wale Majaji walioamua kutumika kisiasa. Kwa sababu nyinyi wenyewe mnajua kwamba sina hatia, mnamuadhibu mtu asiye na hatia. Hivyo, nataka niseme jambo moja: Watu wasio na hatia hawaombi msamaha. Wanaoomba msamaha ni wale waliokosa. Huombi msamaha unapokuwa huna hatia. Waheshimiwa Majaji, kwa hiyo, naomba iwekwe wazi katika kumbukumbu rasmi za Mahakama kwamba SIJAOMBA MSAMAHA. Mimi nipo hapa, na Mahakama imekubali kunitia hatiani licha ya kutokuwa na hatia, kutokana na shinikizo na maelekezo ya kisiasa. Mahakama inatumika kisiasa. Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, nataka niwe wazi kabisa kwamba maneno nitakayoyasema yasichukuliwe, kwa namna yoyote ile, kuwa ni ombi la msamaha. Siombi msamaha. Siombi msamaha kwa sababu sina hatia kabisa (I am completely innocent).โ
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
๐ฅนDaah Huyu Jamaaa ๐ซก๐ซก๐ฉ๐๐พ
Mpaka internet inazimwa HUYU NI MWANAUME๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐๐พ
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Kumkuta Lissu na kesi ya kujibu lilikuwa kosa la kwanza kwa mahakama. Hii kutomkuta na UHAINI, lakini ukaanza kutafutatafuta makosa ya UCHOCHEZI, ni kosa la pili, na ni precedent mbaya sana.
Mungu ni mwema -- tutaondoka na huu upuuzi in our lifetime!
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Akiwasilisha mitigating factors, Lissu anasema:
"Historia haijawahi kuwa nzuri kwa Majaji wanaofunga watu wasio na hatia ili wamridhishe mteule. Hilo kosa la uchochezi mmelitafuta wenyewe Majaji kumsaidia mteule wenu."
What a Man!
Gregory mendel Dr.Mr_P ๐ retweeted
Matriculated into the @UniofOxford to read for a Doctor of Philosophy in Law.๐๐ฝ






























