Wale wakongwe tunaomba gari za enzi hizo kwenye comment mimi naanza na Hood from Mbeya to Arusha via Chalinze 2011/2014๐
๐ค Made with AI
Baada ya makamu wa raisi kutangaza kujiuzulu @ayubu_madenge muda huu๐๐๐
Mwalulesa Jr.๐ retweeted
Jamuhuri imejichanganya kwa kumshitaki lisu kwa Uhaini huku ikitumia maneno ya Lissu kuwa โTUTAFANYA UASIโ kama ushaidi kwa kesi ya Uhaini
UASI na UHAINI ni vitu viwili tofauti katika jicho la sheria
Uasi (revolt) ni KUIPINGA serikali
Uhaini (Treason) ni KUISALITI nchi
Note, Nchi si Serikali na Serikali si Nchi
Leo, imekuwa dhahiri kabisa kuwa, Jamuhuri ilikuwa ikiendesha kesi hii kwa danadana za kuiba muda jambo lililozidi kumtesa Lissu mahabusu.
Jamuhuri ilikuwa ikifanya hivi kwa kupeleka mahakamani shahidi mmoja mmoja kila kesi ilipoitwa na saa nyingine Lisu alikuwa anamaliza cross- examination na mashaidi hao saa 5 mchana muda wa kazi wa mahakama ukiwa bado ukitosha kwa shaidi mwingine kupandishwa kutoa ushaidi ili kuokoa muda na mateso ya Lissu.
Lissu akalikemea hili vikali mbele ya majaji na kuwaambia waziwazi kuwa jamuhuri inaidharau mahakama kwa kuwa inajua haina cha kuwafanya.
Ijumaa Jamuhuri ilitoa sababu ya kutomfikisha shaid wao mahakamani kuwa alipatwa na dharula ya kiafya.
โPontius Pilatesโ wakaishia tu kubungโaa kama wanasoma talaka(Namuomba Mungu, huu mwandiko wangu usipate uzito wa contempt of court)
Anyway, Jamuhuri ikaiomba mahakama kuwa leo itamfikisha shaidi huyo pamoja na mashaidi wengine wote waliobaki
Leo kwa shambulio la ghafla, Jamuhuri ikatangaza kuwa haina shaidi mwingine yeyote wa ziada bali ilikuwa ni โdanganya toto kula kunde mbichiโ
Badala yake Jamuhuri ikaeleza kuwa imefunga ushaidi wake lakini kwa guilty conscience ya njia ya Golgota waliyompitisha Lissu, kimaaajabu kabisa katika historia ya criminal proceedings, jamuhuri ikataka kuwahi stand bila nauli
Eti kwa ushaidi wake iliyowasilisha mahakamani ni kama inaona isijielekezee shingo yake kwenye ala ya motion ya prima facie case
Technically ni kama State Attorney alitaka kukwapua majukumu ya DPP ya โNolle prosequiโ yaani kesi iishie hewani bila Lissu kujitetea then kungepatikana political leverage ya jinsi Gavoo ilivyo sikivu na huruma kwa Toto Tundu na pia inakuwa imereconcile na ultimatum ya international community.
Toto Tundu ni Kama akalishitukia bao la mkono alilotaka kufungwa.
Lissu akaja juu kuwa wa kuongelea hoja ya prima facie case ni yeye na hataki mpira kwa kwapani.
Kuwa haiwezekani umshitaki, upeleke mashaidi kisha wewe mwenyewe ndio uwe una hoja ya kuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu au kutojibu.
Lissu akaurudisha mpita ulingoni kwa kifungu cha sheria No 312(1)
Akasema yeye ndiye master of ceremony wa kuwaambia majaji kuwa kwa utopolo uliojazwa mahakamani hana kesi ya kujibu
Yaani ni kama Lissu analazimisha iwe on record kuwa hana kesi ya kujibu sio kwa hisani, bali on merit ili atokee kwenye milango ya Ukonga na sio Tungu
Sasa mpira Lissu keshaurudisha dimbani. Naamini mpaka tarehe 21 kutakuwa na simu chache kati ya pale jirani na Kipunguni A, Pale jirani na ofisi ya taifa ya Takwimu, na pale panaponuka shombo la samaki vibua wakijaribu kutumia โresidual/ filtrateโ best in their possession kuona wanafunikaje pale manyu mwa kuku mbele ya huu upepo mkali?
Great afternoon Daughters and Sons of the abattoir
Kwenye anguko lako tunza tabia ya kila MTU, ili utakapoinuka tena usichanganye kati ya binadamu na wanyama. โ๏ธ
"You'll understand this when you're older:
"perfume ads always feature women, but pain relief ads always feature men."
Nani mwingine kafikia umri usiotaka kona kona nyingi? In short unataka kusikia vitu in terms of numbers, exact time, straight to the point, yes or no na mambo kama hayo !!
But wait who brought the idea of not smiling on the identity card? we all look like rejected sacrifices ๐
๐
Mothers do not fear death.๐
What they fear most is leaving their children behind, knowing that no one will ever love them as they do..
Happy Mother's day, My lovely Mom
Mwalulesa Jr.๐ retweeted
Kwaheri Dkt. Ayub Rioba Chacha. Umetuachia TBC dhoofu.
Sio kazi ndogo kuitumia miaka (10) kugeuza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuwa idara ya uenezi ya tawi la CCM. Shirika ambalo Watanzania wengi sasa hawajisikii fahari kamwe kufuatilia shughuli zake.
Wakati dunia ikikimbizana na teknolojia ya 4K na uandishi wa kiuchunguzi, TBC chini yako ilikuwa 'bize' kuboresha teknolojia ya kusafisha makosa ya serikali kwa kutumia sabuni yenye manukato ya propaganda.
Siku ya uzinduzi wa Meli ya M.V Mwanza, Mtangazaji wa TBC alisema meli hiyo itafanya safari zake katika nchi mbalimbali itakwenda Kenya, Uganda, Burundi, DR Congo, Zambia, Malawi na Sudan Kusini,
Uongozi wa TBC ukajitokeza kutoa ufafanuzi kwamba mtangazaji alichokusudia kukisema ni MV Mwanza itasafฤฑrisha mizigo ambayo baadaye itapakiwa katika vyombo vingine vya usafฤฑri kuzifฤฑkia nchi zilizotajwa.
Pamoja na malezo na ufafanuzi huo kutoka kwa uongozi wa TBC, bado mtamgazaji alichukuliwa hatua za kinidhamu baada ya maneno yake. Hapo ndiyo nilihitimisha mtazamo wangu, Mmechanganyikiwa.
Utetezi wako kuhusu TBC kuonesha matangazo ya mpira (AFCON na WORLD CUP) yasiyokuwa na ubora wa picha kwamba ni fitina tu, ulituonesha sasa umefika kikomo cha kuendelea kuwa Mkurugenzi wa TBC.
Shukrani kwa kuhakikisha TBC haifanyi kazi yake ya msingi kama chombo cha habari cha umma. Ilikuwa kazi ngumu kuhakikisha Watanzania hawapati habari za kweli. Lakini wewe uliishinda changamoto hiyo.
Wakati mashirika ya habari ya serikali kama Al Jazeera (Qatar), NHK (Japan), BBC (UK), DW (German), France 24 (France), ABC (Australia) yanajaribu kujitenga na siasa, TBC ilichagua njia tofauti. Njia ya propaganda.
British Broadcasting Corporation (BBC) haina hofu ya kuikosoa serikali ya Uingereza. Kipindi chao cha Panorama au mahojiano ya asubuhi ya Radio 4 huwabana mawaziri mpaka wanashindwa kujibu.
Waandishi wa BBC hawasubiri tamko la serikali ili kutoa habari; wao ndio wanatafuta habari. BBC inajiona inawajibika kwa walipa kodi, wakati TBC chini yako inajiona inawajibika kwa mteuzi wako na watawala.
Mashirika ya Kimataifa yanalazimika kuwa bora ili visipoteze wasikilizaji. TBC chini yako imejiona haina kitu cha kupoteza kwa sababu ina uhakika wa ruzuku kutoka Serikalini bila kujali ubora wa maudhui.
Wakati mashirika ya utangazaji ya umma huko duniani yanajitahidi kusimamia uhuru wa habari, TBC chini yako iliamua kuwa jukwaa halali la propaganda za Serikali. Nafikiri Ulichagua propaganda kwa kuwa zinalipa..
Umeondoka ukiacha nyuma kivuli cha taasisi kuliko taasisi yenyewe. TBC iliugua kwa muda mrefu, na wewe kama mkurugenzi (Daktari), uliandika dawa ile ile kila sikuโdawa iliyozidisha ugonjwa badala ya kuponya.
Chini ya uongozi wake, TBC ilifanikiwa kwa njia ambazo hakuna mkurugenzi mwingine angeweza: TBC sasa ni runinga ambayo Watanzania hawaitazami. Mafanikio makubwa. Kufikia zero audience si kazi ndogo!
Chini ya uongozi wako, TBC ilifanikiwa kuacha kuwa chombo cha habari na kuwa mdomo wa mapambio. Habari ikianza, unajua tu ni nani amepiga chafya โWhite Houseโ na nani amekata utepe wa choo cha shule.
Umeifanya TBC kukaa mbali na kero za wananchi kama vile muuguzi anavyokimbia mgonjwa wa kipindupindu. Wananchi wanalia kukosa ajira, TBC inakuonyesha kipindi cha maendeleo ya viwanda vya kufikirika
Ni ufundi wa hali ya juu kuiacha TBC mahututi kiasi kwamba hata kulinganishwa na redio mbao ni matusi kwa redio mbao hizo. Leo hii, TBC inazidiwa viewership na 'online garbage media' zenye kamera moja tu.
Umeifanya TBC kuwa chombo ambacho watu wanatazama pale wanapotaka kujua kama kuna โteuziโ au kuna โsalamu za rambirambiโ au labda wanataka kufuatilia gwaride la maadhimisho ya UHURU.
Gari la umma linapaswa kubeba kila mtu: mawazo mbadala, upinzani, na asasi za kiraia. TBC chini yako ilichagua kubeba โwatawala pekee,โ huku ikiwaacha wananchi barabarani na kero zao, watajijua huko.
Tulitegemea ushauri kwamba, Mkurugenzi wa TBC ateuliwe na bodi huru baada ya ushindani wa kitaaluma. TBC, uteuzi ni wa kisiasa, hivyo โderevaโ lazima amsikilize aliyempa gari badala ya abiria (wananchi).
Kuwe na Bodi Huru ya Utangazaji. Wakurugenzi wasiteuliwe na mwanasiasa, bali wafanyiwe usaili na bodi ya kitaaluma. Hii itawapa ujasiri wa kuruhusu habari zenye kukosoa bila hofu ya kutumbuliwa.
Hutakiwi hata kuwasuta hao ambao wanakuona/wanakuita โchawaโ. Mazingira ya utendaji shughuli zake TBC ukiwa Mkurugenzi Mtendaji zinasadifu hicho ambacho wakosoaji wako wanakiona kama โuchawaโ
Tulitegemea TBC ikiwa chini yako, kwa muktadha tuliokufahamu nao ukiwa mhadhiri UDSM, lazima iache kufanya kazi kama State Broadcaster (ya utawala) na ianze kuwa Public Broadcaster (ya wananchi).
Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) ilipaswa kuwa Public Broadcaster (inayotumikia maslahi ya umma), lakini sasa inafanya kazi kama State Broadcaster (inayotumikia maslahi ya utawala uliopo).
Kama TBC ingekuwa gari, umeiacha kama gofuโhaina injini wala matairi, lakini inapiga honi za kelele. Ni kitu kilichosimama tu kinachojidai kuwa chombo cha maendeleo. Ni kushindwa kimuundo na kitaalamu.
Martin Maranja Masese (MMM) / Mtikila.
Kipato kinapo ishia kwenye chakula na malazi, kiuhalisia kazi unayo Fanya inakuwa si fursa ya maendeleo, bali ni juhudi za kubaki hai, ambayo ni fursa na maendeleo Kwa muajiri wako. Hari hii ilikuwa na jina lake Karne ya 16, iliitwa Utumwa".
#MwalulesaSenior
Et "Hao waliokutafuta kipindi hiki hao ndio cycle yako" wew uliwatafuta? Au wew ulimtafuta huyo mtu na akashindwa kukujibu? ulitegemea akutafute? ๐ฎAu nyie ndio mna haki ya kutafutwa kwanza...? Tushukuruni tulio hai na pia tuwaombee dua wenzetu waliotutangulia.










