MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector) profile picture

PARADIGMS

Dar es Salaam, Tanzania
Joined August 2017
Photo by MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector)Photo by MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector)Photo by MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector)Photo by MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector)Photo by MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector)Photo by MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector)Photo by MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector)Photo by MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector)Photo by MAK Mringo (PhD) (@SnrDirector)
Ukishamuomba Mungu akakupa umri, utumie vizuri kwa maslahi yako na jamii yako hapa duniani na. akhera
8
47
2
190
Its Paradigms schools and colleges again – at Pemba South, Tanzania
3
404
Asalaam alaykum ya ikhiwatul-muuminuuna. Natumai kwa uwezo wa Allah mmeamka salama salmini. Leo ni mwezi 9 SWAFAR (mfungo tano). Nakuhimizeni pamoja na kuihimiza nafsi yangu, tujitoeni kikamilifu kufanya ibada kadri tutakavyojaaliwa kwani mbora wetu ni muumini anayejitenga na matendo mabaya ba kujinasbisha kwa matendo mema. Nawatakia subhi njema na aljumaa munawwara- in sha Allah !!!! – at Pemba South, Tanzania
2
21
1,044
𝐓𝐡𝐞 𝐎𝐥𝐝 𝐊𝐞𝐲 A retired professor had a habit of locking an old wooden box every night. Inside it were his most precious papers, memories, and a small amount of cash. One day, he misplaced the tiny key. He searched everywhere—his desk, cupboards, bookshelves, even under the carpets. Nothing. He called his son, an engineer. The son came with gadgets, flashlights, and tools. He examined the lock carefully and said, “Don’t worry, Father. I’ll break it open.” Just then, the professor said, “Wait. Let me call my old Schoolmate first.” The son was puzzled. “Why? He’s not a locksmith!” A little later, the old Schoolmate arrived. They smiled, laughed, and began talking about their college days. After an hour, the old schoolmate suddenly asked, “Do you still hide important things inside your old dictionary, like you did in the hostel?” The professor froze. He walked to his bookshelf, pulled out a thick dictionary, and there—between the pages—was the tiny key. The son laughed. “All my engineering tools, and your friend solved it just by knowing you!” The professor smiled and said: “Experts can solve problems. But old friends remember the places where you lose yourself.” 𝐌𝐨𝐫𝐚𝐥 𝐨𝐟 𝐭𝐡𝐞 𝐬𝐭𝐨𝐫𝐲: *Stay connected with people who have known you through different chapters of life.* *Sometimes, they don’t just help you find solutions they help you find parts of yourself you forgot.*
1
223
Wakati wa kufanya dialysis, damu hutolewa mwilini kupitia bomba jekundu, Hupitishwa kwenye mashine ya dialysis, Damu husafishwa uchafu wote wa shuhuli za mwili nakisha kuingizwa tena ndani ya mwili kupitia bomba la blue. Utaratibu huu hurudiwa kwa masaa 4 wakati mgonjwa akiwa ametulia kitandani Utaratibu huo unafanywa mara 3 kwa wiki, nisawa na mara 12 kwa mwezi. NA Kila wakati inachukuwa masaa 4, ambayo ni sawa na masaa 48 kwa mwezi. Kwa wale ambao hawajaathirika, mchakato huu wa kusafisha damu unafanywa na figo moja kwa moja, mara 36 kila siku. Ndani ya mwili wako bila jitihada au usumbufu wowote hata wakati unaendelea na shughuli zako. NB: Mshukuru mungu kwa afya njema, Na uzitunze vizuri figo zako. Inawezekana wengi Tukawa Tunachukulia Uzima na Afya Zetu For Granted, Lakini kama Ukipata Muda wa Kutembelea Wodi hata 2 huku Hospitali Ndio Utaona Uthamani na Umuhimu wa Kuitunza na Kuithamini Afya Yako! JALI SANA NA TUNZA AFYA YAKO! Nashare haya Maarifa BURE yakusaidie kubadilika Kwa swali LOLOTE usisite kuwasiliana nami kupitia WhatsApp namba 👇 0620225203 Dr Anidu
6
37
175
12,272
KUNA JIHADI INAENDELEA MAHALI FULANI *ASSALAMU ALAIKUM WARAHMATULLAHI WABARAKATUH!* *Taarifa ya Utekelezaji wa* *Darsa za Familia* Katika utekelezaji wa maazimio ya Semina ya Wanawake iliyofanyika katika Kituo cha Madrasatul Fath Madala – Lushoto, tunapenda kuwataarifu kuwa wiki hii tarehe *14/06/2026* , sawa na Jumapili, tutaanza utekelezaji wa Azimio la Kwanza, ambalo ni kuanzisha Darsa za Familia katika ngazi za vitongoji. *Mahali* 📍 Nyumbani kwa Mzee Juma (maarufu kwa Mama Suleyman), Madala – Mtaa wa Dodoma. *Muda* 🕥 Saa 10:30 hadi Saa 12:00 jioni. *Mada 1:* Haki na Wajibu katika Familia kwa Mujibu wa Mafundisho ya Kiislamu. *Vipengele vya Mada:* 1. Haki za Mume (Baba) kwa Mke (Mama). 2. Haki za Mke (Mama) kwa Mume (Baba). 3. Haki za Watoto kwa Wazazi. 4. Haki za Wazazi kwa Watoto. *Ndani ya Darsa kutakuwa na Programu ya Malezi na Maendeleo ya Familia.* Kwa kuanzia, kila nyumba itakayofikiwa na darsa hii itakabidhiwa: 1. Muswala mmoja wenye thamani ya Tsh 18,000. 2. Msahafu mmoja wa Qur'an Tukufu. 3. Miche miwili ya matunda, ambayo itapandwa na washiriki wa darsa na kutunzwa na familia husika. *Motisha na Ufuatiliaji* Ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira, kujenga utamaduni wa maendeleo na kuwajengea familia moyo wa uwajibikaji, zawadi maalumu zitatolewa kwa familia zitakazoonyesha juhudi kubwa na mafanikio katika utunzaji wa miti hiyo. *Malengo ya Programu* 1. Kuimarisha maadili ya Kiislamu ndani ya familia. 2. Kukuza malezi bora ya watoto. 3. Kuimarisha mahusiano mema kati ya wazazi na watoto. 4. Kuhamasisha ibada na usomaji wa Qur'an katika familia. 5. Kukuza utunzaji wa mazingira kupitia upandaji wa miti ya matunda. 6. Kujenga familia zenye mshikamano, uwajibikaji na maendeleo endelevu. Tunawaalika ndugu wote kushiriki katika darsa hii muhimu kwa ajili ya kujenga familia bora, jamii bora na kizazi bora kwa idhini ya Allah (S.W.T). "Kila mmoja wenu ni mchungaji, na kila mmoja ataulizwa kuhusu anaowachunga." *Imetolewa na,* Mudeer, Hatibu Kigoda *Madrasatul Fath Madala Lushoto @The Connected Aid* NINI MAONI YAKO?
1
132
Asalaam alaykum ya ikhiwatul-muuminuuna. Natjmai kwa uwezo wa Allaah mmeamka salama salmini. Leo ni mwezi 1 MUHARRAM (mfungo nne). Ninawatakia kheri ya mwaka mpy wa kiislam. Nawasihi pamoja na kuisihi nafsi yangu;- tuutumieni vyema mwezi huu mtukufu kwa kufanya ibada na mambo mema kwani mbora miongoni mwetu ni yule amchae Allah. In sha Allah nawatakia subhi njema na tafakuri njema ya namna ya kuuendea mwaka huu!!!!
1
138
Je, Jamaa Wanaweza Kupewa Zakkaah? Ndiyo, ikiwa: •ni maskini, •na si katika wale unaowajibika kuwahudumia moja kwa moja. Kuwapa ndugu: •kuna thawabu ya Zakkaah, •na thawabu ya kuunga undugu. Mtume ﷺ amesema: “Sadaka kwa ndugu ni sadaka na kuunga undugu.” [Sunan At-Tirmidhiy] ⸻ Watu Wasiostahiki Kupewa Zakkaah Kwa ufupi: •matajiri, •wenye uwezo wa kujikimu, •wazazi wako, •watoto wako, •na mke wako, hawapewi Zakkaah yako kwa sababu tayari una wajibu wa kuwahudumia. Na hili tutalifafanua zaidi katika darsa ijayo In shaa ALLAH. ⸻ Makosa Yanayofanywa Na Watu 1. Kutoa Kwa Marafiki Tu Wengine huwapa watu wanaowapenda hata kama si wahitaji. ⸻ 2. Kuwapa Matajiri Baadhi huwapa wenye uwezo kwa sababu ya aibu au urafiki. ⸻ 3. Kutotafuta Wenye Mahitaji Halisi Muislamu anatakiwa ajitahidi kuhakikisha Zakkaah inafika kwa wanaostahiki. ⸻ Kauli Za Wanazuoni Imam Ibn Kathir amesema: “ALLAH Mwenyewe ndiye aliyegawa makundi ya Zakkaah, jambo linaloonyesha umuhimu wake mkubwa.” Na Imam Ash-Shafi’i amesema: “Hairuhusiwi kutoa Zakkaah nje ya makundi yaliyotajwa katika Qur’an.” ⸻ Hikma Ya Kugawa Zakkaah Kwa Makundi Haya 1.Kuondoa umasikini 2.Kusaidia wenye shida 3.Kujenga mshikamano wa jamii 4.Kueneza huruma na mapenzi 5.Kuimarisha Uislamu na da‘wah ⸻ Nasaha;- Ewe Muislamu, unapotoa Zakkaah: •usitazame ukubwa wa unachotoa, bali tazama kwa nani kinakusudiwa mbele ya ALLAHﷻ. Huenda dirhamu moja kwa maskini: •ikakufungulia milango ya Pepo, •ikafuta madhambi yako, •na ikawa sababu ya nusura yako Siku ya Qiyamah. ⸻ Hitimisho:- Katika darsa hii tumejifunza makundi 8 yanayostahiki kupewa Zakkaah kwa mujibu wa Qur’an Tukufu. In shaa ALLAH katika darsa ijayo tutajifunza: Watu Wasiostahiki Kupewa Zakkaah. ⸻ والسلام عليكم ورحمة الله وبركاته. Ni mtumishi wenu Abuu Hafswah Haruna Jumanne Kapama Twabuuri
106
Amka na Abuu Hafswah “assalaam alaykum warahmatuLLaHI wabarakaatu” Darsa Ya Tisa:- Wanaostahiki Kupewa Zakkaah Kwa Mujibu wa Qur’an, Sunnah na Kauli za Wanazuoni ⸻ Utangulizi AlhamduliLLAH Rabbil-‘Aalamiyn. Tunamhimidi ALLAHﷻ kwa neema ya Uislamu na kwa kutufundisha hukmu za dini yetu. Rehma na amani zimshukie Mtume wetu Muhammad, ahli zake, maswahaba zake na wote wanaofuata uongofu wake mpaka Siku ya Qiyamah. Katika darsa zilizopita tulijifunza: •maana ya Zakkaah, •masharti yake, •aina za mali zake, •na namna ya kuitoa. Leo, kwa idhini ya ALLAHﷻ, tutajifunza: Wanaostahiki Kupewa Zakkaah. Hii ni mada muhimu sana kwa sababu watu wengi: •hutoa Zakkaah bila kujua wanaostahiki, •au huwapa wasiostahiki. ⸻ Dalili Kuu Ya Wanaostahiki Zakkaah ALLAHﷻ amesema: ﴿إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴾ “Hakika sadaka (Zakkaah) ni kwa mafaqiri, masikini, wanaozikusanya, wanaotiwa nguvu nyoyo zao, katika kuwakomboa watumwa, wenye madeni, katika njia ya Allah, na msafiri aliyekwama. Huu ni wajibu uliowekwa na ALLAH”. [Surat At-Tawbah: 60] Aya hii imekusanya makundi 8 yanayostahiki kupewa Zakkaah. ⸻ Kundi La Kwanza Mafaqiri (الفقراء) Hawa ni watu: •wasiokuwa na mali kabisa, au •wenye mali kidogo sana isiyowatosha mahitaji yao ya msingi. Hawa ndio wanaohitaji zaidi. Mfano: •asiye na chakula cha kutosha, •asiye na makazi, •asiyeweza kujisitiri. ⸻ Kundi La Pili Masikini (المساكين) Masikini ni: •mwenye kitu kidogo, lakini hakimtoshelezi. Mfano: •ana kazi, lakini kipato chake hakitoshi kwa familia yake. ⸻ Tofauti Kati Ya Faqiri Na Maskini Wanazuoni wengi wanasema: •Faqiri ni mwenye hali mbaya zaidi. •Maskini ana nafuu kidogo kuliko faqiri. ⸻ Kundi La Tatu Wanaokusanya Zakkaah (العاملين عليها) Hawa ni watu wanaoteuliwa: •kukusanya, •kuhifadhi, •kuandika, •au kugawa Zakkaah. Wanaruhusiwa kupewa ujira kutokana na Zakkaah hata kama wana uwezo wa kifedha. ⸻ Kundi La Nne Wanaotiwa Nguvu Nyoyo Zao (المؤلفة قلوبهم) Ni watu wanaopewa: •ili wavutiwe na Uislamu, •au kuimarishwa katika imani, •au kuzuiwa madhara yao dhidi ya Waislamu. Mfano: •Muislamu mpya dhaifu katika dini, •au mtu mwenye ushawishi anayetarajiwa kuisaidia dini. ⸻ Kundi La Tano Katika Kuwakomboa Watumwa (وفي الرقاب) Zamani Zakkaah ilitumika: •kuwasaidia watumwa wapate uhuru wao. Na wanazuoni wengine wamepanua maana yake katika: •kuwaokoa Waislamu walioko kifungoni kwa dhulma. ⸻ Kundi La Sita Wenye Madeni (الغارمين) Hawa ni watu waliobebeshwa madeni halali na hawawezi kulipa. Mfano: •aliyepata hasara, •aliyekopa kwa dharura ya maisha, •aliyebeba jukumu la kuleta suluhu kati ya watu. Lakini si mtu anayekopa kwa: •maasi, •anasa, •au ubadhirifu. ⸻ Kundi La Saba Katika Njia Ya ALLAH(في سبيل الله) Asili yake ni: •kusaidia jihadi ya haki katika dini ya ALLAHﷻ. Na baadhi ya wanazuoni wamejumuisha: •shughuli za kueneza dini, •elimu ya Kiislamu, •da‘wah, ikiwa kuna haja na maslahi ya wazi. ⸻ Kundi La Nane Msafiri Aliyekwama (ابن السبيل) Ni msafiri: •aliyekatika safari, •akaishiwa na mali, •au akashindwa kufika nyumbani. Hupewa kiasi cha kumfikisha mahali pake hata kama ni tajiri katika mji wake. ⸻ Je, Lazima Kugawa Kwa Makundi Yote 8? Wanazuoni wametofautiana. Lakini wengi wanasema: •inajuzu kumpa kundi moja ikiwa kuna haja kubwa. Mfano: •kuwasaidia mafaqiri wengi katika eneo fulani. ⸻ Nani Anafaa Kupewa Zaidi? Wanaohitaji zaidi: •mafaqiri, •masikini, •wenye madeni makubwa, hupewa kipaumbele. ⸻
110
Laa ilaaha ill_allaahu,wahdahu laa shareeka lah,lahul_mulku_ wa lahul_hamdu,wa huwa 'alaa kulli shay''in qadeer
1
5
80
Life after death is a powerful reminder that this world is temporary. One hour after your funeral, the crying slows down. Your family goes home to take care of guests, while your body is left with the organisms in the soil. By the end of the day, people are already talking about sports, news, and politics again. Your reflexes are gone. Your body begins to cool down. A few days later, your workplace starts looking for someone to replace you. Your body begins to swell. Your skin becomes tight, and your organs begin to turn into liquid. Two weeks later, your family sits with a lawyer to divide what you left behind. Your nails and teeth begin to fall out. Three months later, your spouse laughs again, your children smile again, while you continue breaking down into the earth. A year later, someone visits your grave and says: “It feels like just yesterday.” By then, insects and time have destroyed your burial cloth. Ten years later, a friend sees your video and remembers you for a moment. Only your bones remain. This is how quickly the world moves on. So ask yourself: Who are you really living to please? The people who forget you within days? Or the Creator who remembers you forever?
51
📌 Hadithi: Mwenye uwezo lakini hakuchinja Udh-hiyah asikaribie Swala yetu 🔊 Hadithi Kutoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba Mtume Muhammad ﷺ amesema: «مَن كان له سَعَة، ولم يُضَحِّ، فلا يَقْرَبَنَّ مُصَلَّانا» “Yeyote mwenye uwezo lakini hakuchinja Udh-hiyah, basi asikaribie sehemu yetu ya kuswalia.” [Hadithi Hasan, imepokewa na Ibn Mājah na Ahmad] 📩 Maelezo Abu Hurayrah رضي الله عنه anaeleza kuwa Mtume Muhammad ﷺ amesema: Muislamu yeyote mwenye uwezo wa kuchinja Udh-hiyah lakini akaacha kufanya hivyo, basi asikaribie Swala ya ‘Iyd pamoja na Waislamu. Hii ni kwa sababu haifai kwa Muislamu kuacha ibada ya Udh-hiyah hali ya kuwa ana uwezo wa kufanya hivyo. Udh-hiyah ni ibada kubwa na ni miongoni mwa alama mashuhuri za Siku ya ‘Iyd al-Adh-ha. Wanazuoni wengi wanaona kuwa Udh-hiyah ni Sunnah iliyokokotezwa sana kwa mwenye uwezo, huku baadhi ya wanazuoni wakisema ni wajibu kwa mwenye uwezo. 📩 Maana ya Maneno 🔹 “Mwenye wasaa” Yaani mwenye uwezo wa kuchinja Udh-hiyah. 🔹 “Mswala wetu” Yaani sehemu ya kuswalia Swala ya ‘Iyd. 📩 Faida za Hadithi 1️⃣ Hadithi inaonyesha kusisitizwa sana kwa ibada ya Udh-hiyah kwa mwenye uwezo, na wengi wa wanazuoni wanaona ni Sunnah iliyokokotezwa sana. 2️⃣ Kauli ya Mtume ﷺ: “Asikaribie sehemu yetu ya kuswalia” haimaanishi kuwa Swala yake haitaswihi bila Udh-hiyah, bali ni onyo kali na adhabu ya kunyimwa kukaa pamoja na watu wema. 3️⃣ Mwenye kutokuwa na uwezo wa kuchinja halazimiki kufanya Udh-hiyah. 4️⃣ Ni bora kwa Muislamu asiiache Udh-hiyah akiwa na uwezo, kwa sababu kufanya hivyo humtoa kwenye lawama na hutimiza ibada hiyo adhimu.
2
81
WAZAZI WALIOFARIKI Mzazi anapofariki, kumbuka kwamba umeingia katika hatua mpya ya birr (wema na utiifu) kwa mzazi huyo. Birr baada ya kifo ni amana na moja ya aina za kweli kabisa za wema kwa wazazi, kwa sababu birr wakati wa uhai wao inaweza kuchanganyika na ria, kujionyesha wema mbele yao au kutarajia sifa kutoka kwao au watu wengine. Lakini baada ya kufariki kwao, hakuna anayesikia na kuona unachofanya isipokuwa Allah. Mzazi aliyefariki ana uhitaji mkubwa zaidi kwa watoto wake kuliko hata alipokuwa hai. Yale ambayo watoto huwafanyia wazazi wao wakati wa maisha yao mara nyingi ni kwa ajili ya mahitaji ya dunia. Lakini baada ya kifo, ni Allah pekee ndiye anayejua yaliyo mema au mabaya yanayomsubiri marehemu kaburini. Du’a — yaani kumuomba Allah — amrehemu marehemu na amshushie rehema Zake, ni jambo lenye thamani kubwa sana kwa aliyefariki. Kupitia du’a ya mtoto, Allah kwa fadhila na rehema Zake hulitia nuru kaburi, huondoa giza lake, hulipanua na kuondoa mateso yake. Na Allah hulifanya kaburi kuwa bustani miongoni mwa bustani za Peponi kwa marehemu. Ikiwa wazazi wako bado wako hai lakini si Waislamu, basi mojawapo ya matendo makubwa ya upendo na birr ni kumuomba Allah awaongoze kwenye Uislamu. Muombe Allah afungue nyoyo zao kwa haki, awape uelewa na awawezeshe kutambua rehema na upweke Wake. Uongofu ni zawadi kubwa zaidi unayoweza kumtakia mtu unayempenda — hasa wazazi wako — kwa sababu unawanufaisha duniani na Akhera. Endelea kuwaonyesha wema, subira na tabia njema, kwani upendo wa kweli na mwenendo mzuri ni miongoni mwa njia bora za da’wah. Kwa hiyo, daima wakumbuke wazazi wako waliotangulia mbele ya haki, na muombe Allah awashushie rehema, alitie nuru kaburi lao na kulipanua. Kwa mfano, unapokaribia kula chakula, fikiria ni mara ngapi mama yako alikuandalia chakula kizuri na kukuhudumia maisha yako yote. Hakika moyo wako utalainika, na wakati huo huo ruhusu hisia hizo zikuchochee kumlisha yatima, mjane, mwanamke aliyeachwa au mtu mwenye uhitaji kwa niaba ya mzazi wako aliyefariki, huku ukimuomba Allah awape thawabu zake. Toa sadaka kwa niaba yao ukikumbuka neema nyingi walizokufanyia. Usiwahi kuwasahau wazazi. Haijalishi walikuwa wakali kiasi gani kwako, Allah pekee ndiye anayejua upendo waliokuwa nao mioyoni mwao kwa ajili yako. Wakumbuke katika du’a zako wakati wa kusujudu, kati ya adhana na iqama, katika ibada zako zote na kila wakati. Toa sadaka kwa niaba yao kwa siri, futa machozi ya mayatima, wajane na waliotalikiwa kwa kuwasaidia kwa niaba ya wazazi wako. Wape wenye kiu maji kwa niaba yao, kama vile kuchimba kisima. Jitahidi kuwa mtoto bora kwa wazazi wako, kwani wamejitolea mengi katika kukulea. Hii ndiyo du’a ya kuwaombea wazazi: رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا Rabb-ir-ham-huma kama rabbayaani sagheera ( Qur’an Surah Al-Israa 17:24 ) Maana yake: “Mola wangu! Warehemu wazazi wangu kama walivyonilea kwa upendo nikiwa mdogo.” Mwisho, tuwafundishe watoto wetu du’a hii — kwani siku moja sisi sote tutaikumbuka na kuihitaji.
1
80
HABARI ZA ASUBUHI EWE KIPOFU MWENZANGU Siku moja Imam Ahmad bin Hanbal ndiye alikuwa imam wa msikiti ambao ulikua umefurika waumini wengi. Waumini wakamuuliza: "Ewe Imam, wauona wingi huu wa watu waliokuja kuswali?" Akasema: "Hapana, sijaona hata mtu mmoja". Kwa mshangao mkubwa, mmoja wao akamuuliza: "Je, wewe ni kipofu mpaka usiwaone?" Swali lile lilikuwa na utovu wa adabu na heshima kwa Imam, lakini Imam Ahmad akawajibu: "Kipofu ni yule anayefumba macho yake asimuone mjane aliyeelemewa na mzigo mzito. Kipofu ni yule anayeelekea Qibla lakini akawageuzia mgongo yatima na masikini. Kipofu ni yule anayemsujudia Allah, lakini akawafanyia kiburi waja wake. Kipofu ni yule aliyesimama katika safu za wenye kusali lakini haonekani katika safu za wenye njaa na wasema kweli. Kipofu ni yule anayetoa sadaka siku moja, wakati ana uwezo wa kutoa sadaka kila siku. Kipofu ni yule anayefunga kuacha kula, lakini hafungi kuacha ya haramu. Kipofu ni yule anayeizunguka Nyumba Tukufu ya Makkah, lakini anasahau kuwazungukia masikini wanaokufa kila siku kwa ukali wa uhitaji. Kipofu ni yule anayenyanyua juu sauti ya adhana, lakini hajawanyanyua wazazi wake. Kipofu ni yule anayesali na kufunga, lakini anafanya udanganyifu wakati wa kuuza na kununua. Kipofu ni yule anayesimama mbele ya Allah huku moyo wake ukiwa umebeba kinyongo, chuki, inda na dharau dhidi ya ndugu zake Waislamu. Kipofu ni yule ambaye kuna tofauti kubwa kati ya ibada zake, tabia zake na namna anavyoishi na watu. Kipofu ni yule anayeswali, akasujudu na kufunga, lakini anadhulumu na kutetea dhulma na uonevu. Kipofu ni yule anayesali na kufunga, lakini mikono yake imejaa damu za Waislamu. Kipofu ni yule anayesali, lakini swala zake hazimfai. Kipofu ni yule anayechukua baadhi ya mambo ya dini, akaacha mengine. Amesema kweli Allah Mtukufu pale aliposema: "Na aliyekuwa hapa (duniani) kipofu (kwa kutoiona haki) basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa aliyeipotea zaidi Njia", (Surah, Al-Israai, 17: 72)." Ukweli na ufasaha wa jibu hilo la Imam uliwafanya wote wakae kimya, kwa maana hakuna yeyote aliyesalimika na mapungufu au makosa. Hii ndiyo hali halisi iliyopo hata leo. Kila mmoja wetu akisoma hapa atakubali kwamba kuna eneo ambalo yeye ni kipofu. Tunamuomba Allah ayape nuru macho yetu, na ayafanye yale tunayoyajua kuwa mtetezi wetu siku ya Mwisho na yasiwe kinyume chake dhidi yetu. "Na miongoni mwenu kuwe na kundi linalolingania kheri na linaloamrisha mema na kukataza maovu. Na hao ndio waliofaulu," (Al-'Imran, 3: 104).
1
77
Kumtembelea mgonjwa ni jambo lenye thawabu kubwa katika Uislamu, na lina adabu (maadili) maalum ili kumfariji mgonjwa na kuepuka kumletea usumbufu. Hizi hapa adabu na staha muhimu: 1. Kuwa na nia njema Nenda kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu na kumtia moyo mgonjwa, si kwa mazoea au udadisi. 2. Kutoa salamu na dua Unapoingia, toa salamu kwa upole: “Assalaamu ‘alaykum” Kisha muombee dua, kama: “La ba’sa, tahuurun in shaa Allah” (Hakuna shida, huu ni utakaso kwa idhini ya Allah) 3. Kukaa muda mfupi Usikae muda mrefu hadi kumchosha mgonjwa, isipokuwa kama yeye mwenyewe anahitaji uwepo wako zaidi. 4. Kuzungumza maneno ya faraja Mpe moyo, mfariji, na mtie matumaini. Epuka kumkatisha tamaa au kumkumbusha mateso. 5. Kuepuka maswali mengi Usimuulize maswali mengi yanayoweza kumchosha au kumkumbusha maumivu yake. 6. Kushusha sauti Zungumza kwa sauti ya chini na yenye utulivu ili kumheshimu mgonjwa na mazingira. 7. Kutoleta usumbufu Usiende na kundi kubwa bila sababu, wala kufanya kelele au mambo yatakayomkera mgonjwa. 8. Kumtia moyo wa subira Mkumbushe umuhimu wa subira na malipo yake kwa Mwenyezi Mungu. 9. Kuomba dua ya kupona Muombee kwa dua kama: “Allahumma Rabban-naas, adh-hibil-ba’sa, ishfi anta-shaafi…” (Ewe Mola wa watu, ondoa maradhi, mpe shifa, Wewe ndiye Mponyaji) 10. Kuheshimu hali yake Kama mgonjwa yuko katika hali ya kupumzika au hawezi kuongea, usimsumbue — unaweza kuacha salamu au dua kimya kimya. Kwa kifupi, lengo kuu ni kumfariji mgonjwa, kumpunguzia mzigo wa nafsi, na kumkumbusha rehema za Allah. Hii ni dua fupi na nzuri ya Kiswahili ya kumwombea mgonjwa: “Ewe Mwenyezi Mungu, muondolee maradhi huyu mgonjwa, mpe afya njema, na umtie nguvu na subira. Hakika Wewe ndiye Mponyaji, hakuna uponyaji isipokuwa wako. Mponye kwa uponyaji usioacha maradhi yoyote.” Na hii nyingine fupi zaidi: “Mwenyezi Mungu akuponye, akupe nafuu ya haraka, na akurejeshe katika afya njema.” Unaweza kuisoma kwa upole ukiwa karibu naye au hata ukiwa mbali.
5
20
777