U S H U N U Z I

Dar es Salaam
Joined May 2009
Hatuponi kwa kuukana ukweli. Hatuponi kwa kuikimbia historia. Hatuponi kwa kujiaminisha haikutokea. Hatuponi kwa kujisahaulisha maumivu. Hatuponi kwa kujifanya tumepona. Hatuponi kwa kuuzoea upweke. Hatupo kwa kuigiza hatumhitaji mtu. Hatuponi kwa kujitenga. Hatuponi kwa kulipiza kisasi. Hatuponi kwa kuwaumiza waliotuumiza. Hatuponi kwa kuwachukia waliotuumiza. Hatuponi kwa kuona wabaya wetu wakiteseka. Tunapona tukiaminiwa tena. Tunapona tukisikika tena. Tunapona tukionekana tena. Tunapona tukijisikia kueleweka. Tunapona tukijisikia ni salama kuwa sisi. Tunapona tukiamini tunapendwa. Tunapona tukiachilia ubaya. Tunapona tukisamehe waliotukosea. Tunapona tukimwamini mtu tena. Tunapona tukiamini mtu huyo anasikiliza. Tunapona tukiamini mtu huyo anaelewa. Tukipona tukiamini tunauishi ukweli na hatujidanganyi tena.
1
8
98
Christian Bwaya retweeted
Replying to @bwaya @k_mjege
Watoto wanaproject uhalisia unaokinzana na delusion tuliyojijengea. Inabidi siku moja tukutane kulijadili hili kwa kina.
1
1
4
153
Ukiweza kutofautisha hisia za ngono na mapenzi uwezekano wa mahusiano unayoyaanzisha kudumu unakuwa mkubwa. Hisia za ngono, tamaa, ni msukumo wa kimwili unaowachochea wanyama kuzaliana. Nzi, pamoja na udogo wake anazo hisia hizi—sexual instincts—ingawa hana mapenzi. Hisia za ngono (tamaa) zikiwa kipaumbele chako, vigumu kuwekeza kwenye mahusiano yanayokutanisha fikra na kuruhusu mikinzano ya mawazo kujenga utambulisho wa pamoja—intimacy. Ukaribu wako na mtu, aghalabu, utalenga kukutanisha miili kuliko fikra, imani na mambo yanayowatambulisha (identities). Utavutiwa na mwonekano, utamtamani, ukifanikiwa kukidhi tamaa za mwili hisia hizo zitapoa. Usipozimudu hisia hizi, kama ilivyo kwa nzi, unaweza kucheza na wengi kwa mpigo—maana huwapendi. Mapenzi, tofauti na hisia za ngono, ndizo zinatutofautisha na wanyama wengine. Ukimpenda mtu unahamia kwenye fikra, imani na misimamo yenu. Upendo unakuchochea kuweka mazingira ya kumwamini, kumfanya kuwa sehemu ya faragha yako, na hivyo unampandisha ngazi ya kumruhusu kukufahamu, kuyafahamu matumaini yako, kuzijua aibu zako. Upendo unakuchochea kujitoa ili kumheshimu, kumstahi na kumfanya kuwa sehemu ya maisha yako. Ukaribu wa kiwango hiki ndio unaochochea muunganiko wa utambulisho wenu (identity) ili kuufanya kuwa mmoja. Huo ndio upendo unaodumu, kwa mujibu wa mshunuzi Sternberg. Ingawa uwezo huu anao mwanadamu, ukishakosa upendo wa mzazi utotoni, inaweza kukuwia vigumu mno kumpenda mtu mwingine au hata kumruhusu mtu mwingine akupende kwa kiwango hiki. Katika mazingira kama haya, watu wengi huishia kwenye hisia za ngono, na uwezekano wa ajali nyingi za mahusiano unakuwa mkubwa zaidi. Mchoro: Akili Ige (AI)
1
13
14
428
Kinachokufanya uwe karibu zaidi na mtu (intimacy) sio ngono. Unaweza kulala na mtu kila siku na bado ujisikie ukaribu wowote. Ngono isiyoanza na kufahamiana inaweza kabisa kuzidisha upweke na hata kuharibu uhusiano wenu. Ukaribu, kwa kawaida, unabebwa na kina cha kufahamiana na mtu unayeamini anakuelewa na hata anaposhindwa kukuelewa bado ana utayari wa kuheshimu mtazamo wako. Kufahamiana na mtu kunaanza na imani kuwa uliyenaye ni mtu salama, mtu unayeamini unaweza kumwambia mapungufu yako, mapito yako, siri zako, na hata majeraha uliyowahi kupitia na bado akaendelea kukuheshimu na kukustahi. Unapokuwa na mtu mwenye tabia zinazokufanya uamini unamjua vizuri, anachokisema ndicho anachomaanisha, unachokiona usoni ndicho kinachozungumza moyoni mwake, anachokuambia ndio ukweli wenyewe, huo sasa ndio unaitwa upendo.
1
11
25
551
Christian Bwaya retweeted
Replying to @bwaya
Kuna siku nilikua najithamini binafsi Nikasema Hivi maisha yangu na mienendo yangu kuna mdada anataka niwe mume wake / au sifa nilizokua nazo na maisha ninayoishi kila siku yanaweza kunifanya Mume / Baba bora Nikatabasamu nikasema hapa inabidi nijitengeneze sana
1
47
Christian Bwaya retweeted
Je, wanaume waoaji wenye malengo ya kuanzisha familia wameisha? Je, soko la wanaume wasiochezea wanawake na kuwazalisha limekuwa gumu? Nachelea kuamini waoaji wameisha. Ingawa hakuna anayelazika kuoa, na watu wana sababu mbalimbali za kuamua kutokuoa, bado wanaume wenye malengo ya kuanzisha familia wapo na unakutana nao. “Shida ni nini?” unauliza swali zuri. Kwanza, viashiria vyote vinaleta taharuki kuwa huenda ‘wewe’ wa hapo kibaruani, supermarket na coffee shop huenda sio mtu halisi. Sura uliyonayo ukiwa baa, huenda sio sura unayoamka nayo asubuhi. Hili linatia mawazo sana. Wanaume waoaji wanakua kama hawana uhakika huyo ‘wewe’ waliyevutiwa nae hapo coffee shop na picha wanazoona mitandaoni ndio ‘wewe’ huyo huyo vipodozi vikiisha? Je, kamera ikikosa ubora utabaki na urembo huo huo? Sio kwa ubaya lakini sura yako halisi haifahamiki. Kingine kinachotia mashaka zaidi ni urahisi wako. Hujui kumzungusha mtu aone unahitaji muda kufikiria ombi. Unasema wanaume wenyewe hawa wahuni siku hizi. Ukijivuta vuta harudii tena. Hata wahuni kuna saa nao wanapenda kusikia uko bize kidogo na jambo fulani na kuonana na wewe ni mipango. Mwenzetu siku hiyo hiyo tayari unatandika hadi kitanda na unaosha kabisa mabakuli kwa mwanaume kwa nini asiogope? Lakini kibaya kingine ni kukosa kwako kiasi. Kijana kakuita mzungumze mfahamiane kidogo kabla hajaamua kutoa ratiba ya hatua ya pili. Unakula utafikiri ulikuwa kwenye mfungo wa kukuombea taifa zima? Halafu hushibi. Unaomba hadi ufungiwe ukamalizie nyumbani. Kijana wako anapata mawazo, hii njaa ya pizza, firigisi na vifumbatio vya kuku muda wote ataiweza? Siku hiyo ndio una dharura ya laki mbili ya karibu, huna bando la kujibu maswali yake. Kweli unaona mtatoboa? Tunapenda maisha ya gharama lakini kiasi ni muhimu. Usinielewe vibaya. Sio kwamba watu wanaingilia maisha yako lakini kuna vitu vinatisha na hatujazoea kuviona. Saa nane usiku mtoto wa kike uko mitaani na wala huonekani kuwa na haraka ukapumzike. Kweli? Haya unasema huwa hulewi lakini kweli ndio umalize bia kumi na hupepesuki? Huoni unamtisha kijana wa watu? Inaogopesha ati. Huyu mtu anayegida mvinyo mkali hivi kuna mahali tutaenda au abaki kuwa chombo cha burudani? Ujue hata walevi wanaogopa walevi. Wanaume waoaji wapo wewe ndio unajiamulia mambo. Samahani sana kwa kukuambia ukweli.
10
16
482
Christian Bwaya retweeted
Bwana kaka wikiendi inaendaje? Naomba usinielewe kama mtu ninayejipa jukumu la kukushauri kitu usichokihitaji. Sina hata cha maana cha kukuambia na unajua sisi washunuzi kiutaratibu haturuhusiwi kushauri. Naomba uniruhusu tuongee tu kidogo kama namna ya kutafakari mipango ya kimaisha na familia kwa ujumla. Umri huo umeenda ndugu yangu na maswali najua yamekuwa mengi. Hupendi uulizwe ulizwe na kila ukiulizwa utetezi umekuwa ni ule ule, “Wanawake wa siku hizi hawana sifa za kuwa mke. Sioni wa kumuoa.” Kwanza, tuelewane vizuri hapa mwanzoni kuwa hili, kwa vyovyote, halikusudiwi kuwa shinikizo la wewe kuoa. Una haki kabisa ya kutokuoa na hakuna kitu mtu atakufanya. Unachokosea ni kusingizia wanawake wa kuoa hawapo. Hapo unapojitetea kuwa wanawake wazuri wenye akili ya kujenga familia hawapo ndo unakosea. Ukweli ni kwamba wanawake wazuri wapo wengi. Shida ni wewe. Samahani lakini kama nakushambulia sana. Tuanze na namna unavyoyafikiria mahusiano. Nani kakuambia mkishakutana na mwanamke agenda lazima iwe ngono? Kwa nini unafikiri kinachomwuunganisha mwanaume na wanamke ni ngono? Kama huna kingine unachowaza kwa mwanamke zaidi ya tamaa za mwili unafikiri mwanamke gani wa maana atakuheshimu? Ukiingia kwenye mahusiano kazi yako kubwa ni kuomba utumiwe picha, usifie sura, ujimalize, unafikiri mwanamke anayetaka mume atakuelewa? Hapo ndio unakosea. Unaogopa kuoa vibaya mno na wanawake wa kuoa huwaoni lakini kuzaa wala huogopi. Huoni shida ni wewe bro? Unarahisisha malezi au unakimbia wajibu? Halafu kuna hili la mipango. Mbona kama huna maono? Tukikuuliza umekuja hapa duniani kufanya nini una majibu? Hilo unasema gumu na jua linawaka sana. Tubadilishe swali unataka nini kitokee kwenye maisha yako miaka 10 ijayo? Hujui. Muda wote unatafuta ‘odds’ za kubeti na bado unasema unataka ‘msaidizi?’ Unataka kuwa kichwa cha familia lakini huna cha maana unachojifunza zaidi kufuatilia usajili ya timu za soka Ulaya. Kusoma vitabu na kujifunza ujuzi wowote utakaokuingizia kipato muda huna lakini unajua maisha ya ‘mastaa’ wote. Utapata mke wa kumuongoza kweli kaka? Kingine ni kufikiri mke mzuri ni yule asiye na ndoto wala kufikiri mambo makubwa. Hapa sasa najua nitakuudhi lakini tuvumiliane kidogo nimalizie. Nani amekuambia uanaume maana yake ni kumkandamiza mwanamke na kuhakikisha hafanikiwi? Kwamba ukiona mwanamke anafurukuta kidogo fanya kila unaloweza asifanikiwe. Unafikiri kweli mwanamke gani mwenye akili atakubaliana na wewe? Ndio maana unaishia kuchati na wanawake wasio na mbele wala nyuma asubuhi mpaka usiku mkiulizana, “Uko wapi?” “Uko na nani hapo?” “Unafanya nini?” “Umelala kuelekea wapi?” “Hebu video call nikuone!” Huoni ndio maana unachokwa na wanawake wanaojitambua? Unasema wana dharau ila sio siri kubadilishana ujinga kunachosha. Mwanaume wa dunia ya sasa ngumu sana kutegemea udhaifu wa mwanamke na akatoboa kwenye mahusiano. Wanawake siku hizi wameamka. Wanawake wanapambana. Wanawake wanafikiri mambo makubwa na hawajioni wakiishia kufuatilia tamthilia wakimsubiri mwanaume akatafute. Ukiwa mwanaume anayefikiri mwanamke mzuri ni tegemezi dunia ya sasa itakukatisha tamaa. Sasa hivi lazima ujifunze usawa katika mahusiano. Usawa, hata hivyo, haumaanishi kufanana. Usipobadili fikra ukaelewa kuwa sote, bila kujali jinsi(a), tunastahili heshima sawa, hadhi sawa, fursa sawa, utawalaumu sana wanawake. Samahani sana kaka kwa kukuharibia wikiendi.
1
11
2
21
456
Christian Bwaya retweeted
Wazee wetu waliooana na watu wanaowafahamu, watu wanaojua familia zao, ambao mara nyingi walitoka kijiji kile kile au kijiji cha jirani. Ungesema una mchumba, timu ya upekuzi ingeingia kazini kuchunguza kule ulikoona kuna historia gani kisha ingefanya maamuzi na wewe ungeheshimu. Nyakati nyingine wazee ndio walioamua wangependa kuungana na ukoo upi na kijana wao angetumika kama kiungo. Ndoa ilianza na kufahamiana kwa kina. Lakini pia, mfumo wenyewe wa mahusiano uliruhusu watu kuishi pamoja, kuzungumza na kufahamiana kwa kina. Watu walitofautiana na hata kugombana kama namna ya kuunganisha mitazamo na mazoea kwa njia zisizoleta madhara makubwa. Hata pale tofauti zilipovuka mipaka jamii ilikuwa na mfumo rafiki kuwasuluhisha vijana na mfumo huu ulikuwa na mamlaka yanayoaminika na wengi. Migogoro, kwa msingi huo, haikuachwa imani ibaki kuwa jambo binafsi la mtu mwenyewe na ‘zimwi’ lake. Kizazi chetu siku hizi kimepata ‘exposure’ kumaanisha tunakutana na watu wengi tunaowafahamu lakini hatuwafahamu. Imekuwa rahisi sana kuonana na watu tunaotofautiana sana lakini bado tukiamini tunafanana—tunafikiri kwa vile tumesoma shule ile ile, tunakula chakula kile kile, tunaongea Ki’ngreza kile kile basi tunafahamiana. Hatuogopi kuanzisha mahusiano leo na tukamaliza kila kitu leo leo. Tuna ‘exposure’ kubwa kiasi kwamba tunaweza kuishi miaka miwili na wazazi hawana habari kwamba ‘tunafahamiana’ na mtu asiyefahamika. Kingine, maisha yenyewe hayatupi nafasi ya kukaa pamoja kama familia, kuzungumza na kufahamiana. Hata pale tunapozungumza, kinachotawala ni mipango ya kazi na kushindana na marafiki kutafuta pesa na kuzitumia. Hatupati muda wa kufanya mazungumzo ya kina, yanayotuanika kwa wenza wetu wajue nje ya ndoto za vitu na mali, tunatamani nini. Hatuna muda wa kuelewa zile hisia zetu za kina, matokeo yake tunabaki na mzigo mkubwa wa upweke na hisia zisizozungumzwa. Tunaishi maisha bora kuliko wazazi wetu lakini yenye hasira zisizozungumzwa zikaisha, tunaishi na wivu usiotafutiwa ufumbuzi matokeo yake tunaishi na hatia, majuto, chuki na visasi. Muda wa kupooza maumivu haya ni kama haupo maana muda wote tunafukuzia ‘makataa’ ya kazi (deadline) na vikao vya kupiga dili tuonekane tumefanikiwa! Katikati ya haya yote bado tunajiuliza kwa nini siku hizi ndoa zimekuwa za kifahari lakini hazidumu na wanandoa hawaogopi kuuana na hata wale wanaoishi pamoja ni waaminifu zaidi kwa mabaa medi, michepuko na wanasiasa kuliko kwa wake/waume zao.
8
23
1
48
1,532
Christian Bwaya retweeted
Hatuishi ndio maana tunaogopa kufa. Tunawachukia watu kwa kosa la kuishi ndoto zetu. Tunawachukia watu kwa kuonesha uwezo tusiokuwanao au kutumia vipawa na elimu tusiyoitumia. Tukiziishi ndoto na kusudi la kuzaliwa kwetu kifo kinaacha kutisha. Hatuogopi tena kufa. Tukiishi ndoto zetu, na kutumia vipawa na maarifa tuliyonayo, hatuwi tena na sababu ya kushindana na watu na kuwachukia wanaoishi maisha yao.
1
14
23
624
Christian Bwaya retweeted
Replying to @bwaya
Kabisa! Changamoto nyingine ni jinsi jamii inavyopata taarifa, maarifa kwa sasa. Mitandao kwa mfano inatoa nafasi kubwa kwa watu wenye maumivu kuwa wasemaji juu ya ndoa, mahusiano. Kijana tayari anakuwa ameshalishwa matango ya kutosha kabla ya kukutana na Mwl Bwaya...
1
1
39

Anguko letu mara nyingi lipo hapa: hatuna muda wa kujitathmini kwa haki na kujiuliza tumekosea wapi na tumepatia wapi. Badala yake, tunahamishia mapungufu yetu kwa watu wengine na kujiona sisi tuko sahihi kila wakati. Wakati mwingine, tunachukia watu wanaotuambia ukweli kwa sababu ukweli huo unatukutanisha na upande wetu ambao hatutaki kuuona. Ukweli ni kwamba, kuna wakati tunatendewa vile tulivyo, si kwa sababu watu wanatuchukia, bali kwa sababu ya namna tunavyowatendea. Kabla ya kumlaumu mwingine, tuwe na ujasiri wa kujiuliza: Je, tatizo linaweza kuwa kwangu pia?
1
62