Kidumule retweeted
JE, KANISA KATOLIKI LINAAMINI KATIKA KUNENA KWA LUGHA?
Kwanza kabisa, Mtu aliye na Roho Mtakatifu hatambulikani kwa kunena kwa lugha tu bali anakuwa na mapaji saba ya Roho Mtakatifu yaani:
1. Hekima
2. Akili
3. Shauri
4. Nguvu
5. Elimu
6. Ibada na
7. Uchaji wa Mungu(Isaya 11:2).
Mtu huyo akikubali kuongozwa na Roho Mtakatifu anadhihirisha matunda ya kuongozwa na Roho yaani:
-Upendo
-furaha
-Amani
-Uvumilivu
-Utu wema,
-Fadhili
-Uaminifu
-Upole
-Kiasi (Gal 5:22-23)
Kunena kwa lugha ni ishara ndogo tu ya kuwa na Roho Mtakatifu(1Kor 14:22) na tena ni kwaajili ya wasioamini: "Basi hizi lugha ni ishara,si kwao waaminio bali kwao wasioamini; lakini kuhutubu si kwao wasioamini bali kwaajili yao waaminio." (1Kor 14:22)
Na tena kipaji hicho kipo kwa baadhi ya watu tu kama zilivyo karama nyingine na ni kipawa kidogo na tena cha mwisho kwamaana ni kipawa kisichowafaidia wengine.
"Maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu bali husema na Mungu peke yake maana hakuna amsikiaye na kumuelewa bali hunena mambo ya siri katika roho yake.
Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga na kuwafariji na kuwatia moyo.6'Ila sasa ndugu nikija kwenu na kunena kwa lugha nitawafaidia nini isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu au kwa njia ya hotuba au kwa njia ya fundisho?
Vivyo hivyo na ninyi msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana mtakuwa mkinena hewani tu! Basi msipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye; naye anenaye atakuwa mjinga kwangu, kwasababu hiyo, yeye anenaye kwa lugha na AOMBE APEWE KUFASIRI. KAMA MTU AKINENA KWA LUGHA, BASI NA WANENE WAWILI AU WATATU NA SI ZAIDI, TENA ZAMU KWA ZAMU NA MMOJA WAO ATAFSIRI YALE WASEMAYE.
Lakini asipokuwapo mwenye kutafsiri YULE ANENAYE KWA LUGHA NA ANYAMAZE KATIKA KANISA; ASEME MWENYEWE KWA NAFSI YAKE NA MUNGU TU! Kwaajili ya hayo ndugu, takeni sana kuhutubu wala msizuie kunena kwa lugha, lakini mambo yote NA YATENDEKE KWA UZURI NA KWA UTARATIBU!" (1Kor 14:2-4-6.9.11.13.27.28.39)
Katika maandiko hayo, wenye kunena kwa lugha ni kwa faida yao pekee maana wale wanaowanenea hawajui wala kutambua linenwalo.
Kadiri ya mtume Paulo, tunapaswa kuomba na kutaka vipawa vitakavyotusaidia kufaidiana na hasa upendo (1Kor 12:31-13:8;14:1).
Mwanzo wa kanisa walihitaji sana kuona ishara ya kunena kwa lugha ili kuamini kwamba kweli wamepokea Roho Mtakatifu. Siku hizi hatuhitaji ishara hii ili kuamini kwamba tumempokea Roho Mtakatifu.
Wakati wa Yesu miujiza ilikuwa ya lazima kwani Wayahudi hawakuamini neno lolote pasipo ushuhuda na ishara. Ndio maana mahali pengine wanamuuliza Yesu 'UNAFANYA NENO GANI ILI TUAMINI?'
Pamoja na miujiza waliyofanyiwa, bado wengine hawakuamini. Na kwasababu walitegemea sana miujiza, Yesu aliona wanabaki zaidi kwenye mambo ya nje na ndio maana akawaambia Kizazi hiki kinataka ishara ila hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.
Yesu anasema hivi kuonyesha kwamba miujiza ilikuwa njia tu ya kuwadhihirishia kuamini na hivyo miujiza ambayo iliyokwishafanyika iliwatosha kuamini.
Hivyo kunena kwa lugha sio ishara YA LAZIMA katika Kanisa ili kuonyesha uwepo wa Roho Mtakatifu. Ikiwa ishara hii ni ya lazima kudhihirisha kwamba mtu amempokea Roho Mtakatifu, basi na ishara ya NJIWA aliyemshukia Yesu alipokuwa akibatizwa (ambayo ni ishara pia ya Roho Mtakatifu) nayo pia tuitake itokee na kwetu ili tuamini tumempokea Roho Mtakatifu. Tusing'ang'anie tu kunena kwa lugha!
Hata hivyo, baadhi ya waliopo katika chama cha Karismatiki Katoliki hudhihirishiwa karama hii ya kunena kwa lugha. Lakini kama nilivyosema mwanzo kwamba kunena kwa lugha sio ishara ya LAZIMA kwamba mtu anaye Roho Mtakatifu.
Kwahiyo Kanisa linafundisha kwamba si vizuri sana kung'ang'ania na kupendelea vitu ambavyo hatuvielewi vizuri wala kuweza kuvithibitisha kuwa vimetoka kwa Mungu au la, bali tuchuchumilie katika kuyatekeleza yaliyo mema ambayo yanadhihirisha uwepo wa Mungu. Upendo hushinda yote!
TUMSIFU YESU KRISTO.
Kidumule retweeted
LUHAGA MPINA AKATAA UCHAWA MKUTANO MKUU WA CCM
Wakati wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM leo wakiwa wanamshangilia Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kupitisha azimio awe mgombea urais wao 2025, Luhaga Mpina alitulia bila kushangilia.
Pia Mpina hakuvaa nguo za kijani kama za makada
Kidumule retweeted
Wabongo hawana dogo!!!
Nimecheka sana 😂😂😂
Wajumbe wa Mkutano Mkuu tukumbuke, kula ni kule lakini kura ni Kwa TAL
Kidumule retweeted
"Kwenye maisha ni muhimu sana kudhibiti hasira. Hasira hufanya ulimi kuwa mwepesi kuliko akili, Yapitayo kwenye ulimi hayarejei." ~Togolani Mavura.
Kidumule retweeted
PARIPESA pesa nje nje🏆🦅
➡️ 1NZ6T
320 odds
➡️ TYK6T
14 odds
➡️ RZU6T
6 odds
➡️ A5Y6T
10 odds
➡️ 5AL6T
11odds
JISAJILI na Paripesa,ili tushinde wote na leo tena ,Mlioshinda jana Big up🫡
➡️shorturl.at/fuJK0
Promo code jaza👉🏿KIRIKUU
Ili upewe bonus yako.
Kidumule retweeted
Warangi mnasehemu yenu Peponi
Mke lazima awe rafiki yako
Mke lazima awe mshauri wako
Mke lazima awe msaidizi wako
Mke lazima awe mlinzi wako
Mke lazima awe mpambe wako
Mke lazima awe mpiganaji wako
Mke lazima awe mlezi wako
Mke lazima awe ubavuni mwako
Mke lazima awe na misimamo yako
Mke lazima awe na maono yako
Mithali 18:22
"Apataye mke apata kitu chema"
Msimamo wa Mwl.Regina kukataa unafiki wa kukutana na maadui wa mume wako msibani,umefanya Edward atabasamu huko aliko akisema nimeacha Jembe.
Kwa heri NGARASH-MONDULI
Kidumule retweeted
Katika hali isiyo ya kawaida, mlinzi katika msafara uliobeba mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa, amempiga ngumi mwananchi aliyekuwa amesimama kando ya barabara kuaga mwili huo.
Tukio hilo limetokea leo eneo la Ngarenaro mkoani Arusha wakati mwili huo ukisafirishwa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwenda Kijiji cha Ngarash, wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Kidumule retweeted
⚠️Kama uko rough in driving na hauna mapenzi ya kutosha na gari achana na Nissan Dualis..
.
Nissan Dualis ni mtoto wa ushuani shuruba za Chanika maji matitu haiwezi..
.
Ile gari inafaa sana wadada hasa bankers, wamama na wazee/vijana wasitaarabu..
.
Tofauti na hapo utakitesa tu..
Kidumule retweeted
#Aina ya Hati za Kusafiria za Tanzania – at Dodoma, Tanzania
Kidumule retweeted
"Ukiishi vizuri na watu mitandaoni na nje ya mitandao hata usipokuwepo kwenye kusanyiko la watu hatakosekana walau yule mmoja wa kusema jamani 'Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni." ~Togolani Mavura.
Kidumule retweeted
I am deeply saddened to learn of the passing of the President of Namibia, His Excellency @hagegeingob, a dear brother, a venerable Pan Africanist and a great friend of Tanzania.
On behalf of the people of the United Republic of Tanzania, I send my condolences to the people of the Republic of Namibia, the Acting President, His Excellency Dr. Nangolo Mbumba, Madam First Lady, Her Excellency Monica Kalondo, family, friends and comrades in SWAPO.
May you all be comforted during this difficult time. May his soul rest in peace. Amen.
Mt. Ritha wa Kashia, UTUOMBEE
HISTORIA FUPI YA MTAKATIFU RITA WA KASHIA, MTAWA
Rita alizaliwa Roccaponera karibu na Mkoa wa Umbria huko Italia Jumamosi tarehe 22 Mei 1381 akiwa mtoto pekee wa wazazi wake. Aliolewa akiwa na miaka 15 japo alitamani sana kuwa mtawa, lakini aliwatii wazazi wake akakubali.
Mume wake alikuwa tajiri lakini mwenye kiburi na hasira za haraka. Hivyo Rita alipata magumu katika ndoa yake. Walizaa watoto wawili wa kiume. Alimvumilia mumewe na daima hakuchoka kumwombea yeye na wanawe.
Katika mwaka wa 18 wa ndoa yake mume wake aliuawa katika ugomvi. Watoto wake hao wawili wa kiume walipokua, walinuia kulipiza kisasi kwa kifo cha baba yao. Jambo hili liliuongeza uchungu wa Rita, mama yao. Aliomba sana ili wasilifanye hilo jambo waliloazimia. Sala yake ilisikilizwa na Mungu. Wanawe hao waliugua kiasi cha kutoweza kulipa kisasi. Baadaye walikufa katika hali ya neema, tena walimsamehe aliyemwua baba yao.
Mume wake na watoto wake walipofariki, Rita alijiunga na shirika la Mt. Augustino na ilikuwa baada ya mapingamizi mengi na kukataliwa, alijikuta ndani ya monasteri Kimiujiza. Ndiyo maana hata leo ni mwombezi wa mambo Yaliyoshindikana. Katika konventi aliwatii wakuu wake. Alionyesha huruma na wema kwa jirani hasa kwa watawa wenzake waliokuwa wagonjwa. Kwa sala zake aliwaongoa Wakristo wazembe, na wengi walitubu kwa kuona mifano yake.
Tangu utoto wake alikuwa na ibada maalum kwa mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo. Pengine akiyatafakari, roho yake ilishikwa kabisa na mambo ya mbinguni, kiasi kwamba viungo vyake vililegea, na fahamu ikampotea. Siku moja aliposikia hotuba kuhusu Taji la Miiba la Yesu, alijiona kana kwamba alikuwa amelivaa taji hilo. Kweli baadaye alipata donda kubwa kwenye paji la uso. Kwa sababu ya donda hilo alitengwa na wenzake.
Inasemekana kwamba lilipona mwaka 1450 alipokwenda kuhiji Roma, lakini baada ya kuhiji lilimrudia tena.
Kitu cha kushangaza ni kwamba, alifariki dunia, tarehe na siku ile ya kuzaliwa yaani 22 Mei 1457. Alitangazwa Mtakatifu tarehe 24 Mei 1900 na Papa Leo XIII.
MT. RITA WA KASHIA UTUOMBEE
NB: Mtakatifu Rita wa Kashia ni msimamizi na mwombezi wa mambo yaliyoshindikana. Nawaalika tusali Novena kwa Mtakatifu Rita. Tutasali NOVENA ya siku 9. Pengine una nia unayomwomba Kungu na kibinadamu unaona haiwezekani, umekata tamaa. Wengi waliokata tamaa wamepata miujiza mingi kwa Ni ena hii. Weka lengo la kusali kwaajili ya nia yako maalum unayoomba kwa Mungu kupitia maombezi ya Mt. Rita wa Kashia.
2
93



























