officialmuce retweeted
"Akina baba, acheni kunyanyasa akina mama na kuharibu raslimali bora kuliko zote, yaani watoto, tunapata watoto ambao ni mzigo na baadaye tunapata tabu kuwafundisha’...Kamishna- Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa, aliyemuwakilisha Katibu Mkuu @wizara_elimuTz @akwilapo
#MwanzoMzuri
officialmuce retweeted
"Natoa wito kwa washiriki wa mafunzo haya, kuendelea kujifunza siku hadi siku, kuwa wabunifu, na kuambukiza maarifa haya kwa walimu wengine katika Wilaya zao ili manufaa haya yaweze kuwafikia pia"...Dkt. Evaristo Haulle Kaimu RASI.
officialmuce retweeted
"Chuo hiki kilianzishwa ili kupata Walimu wa shahada wenye sifa kama suluhisho la upungufu mkubwa wa walimu katika shule za sekondari, Tumetekeleza vizuri hili."...RASI wa Mkwawa Prof. Esther Ndungumaro aliyewakilishwa na Naibu RASI Taaluma, Dkt Evaristo Haulle.
#MwanzoMzuri
officialmuce retweeted
"Ujumbe wa HakiElimu kwenu, Serikali na jamiii kwa ujumla ni kuwa; aina ya jamii tuliyonayo au tutakayokuwa nayo ni akisi ya malezi na elimu waliyopatiwa au watakayopatiwa watoto wetu katika umri wa mwaka sifuri mpaka minane"... Dkt.Kalage-Mkurugenzi @HakiElimu" 1/2
#MwanzoMzuri
officialmuce retweeted
"Kila mmoja awajibike kuboresha elimu ya awali; Vyuo vizalishe walimu bora na watendaji bora watakaosimamia elimu ya awali, Walimu wazingatie mafunzo na wayatumie ipasavyo kuwaandaa watoto, Serikali iweke mazingira wezeshi kwa wadau wote wa elimu. Dkt. John Kalage.
#MwanzoMzuri
officialmuce retweeted
"HakiElimu kwa pamoja na Chuo Kikuu cha VIA tutaendeleza mafanikio ya #MwanzoMzuri na kuunga mkono jitihada za wenzetu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha @MUCE_yetu kuanzisha mafunzo ya Stashahada ya Elimu ya Awali ambayo yataongeza idadi ya waalimu wenye ujuzi Katika elimu ya awali"
officialmuce retweeted
‘Chuo Kikuu Cha VIA cha Nchini Denmark tunaamini, uthubutu, uvumilivu na kuwa na matarajio inasaidia kufikia malengo, tulifurahi kuona walimu wanakaa kwenye mikeka na wanacheza na watoto’.. Dkt. Suma Kaare-Mwakilishi wa VIA.
officialmuce retweeted
"Kilichoyafanya mafunzo ya #MwanzoMzuri yawe na ufanisi ni kufundisha walimu kutambua umuhimu wa walimu na watoto kushiriki michezo kwa pamoja, hii inaongeza hamasa ya mtoto kucheza na inamfanya kujifunza huku akihakikishiwa ulinzi"... Dkt. Jacqueline Amani - Mhadhiri @MUCE_yetu.
officialmuce retweeted
"Utafiti wa “Mazingira ya Kujifunza na Kufundishia ya Elimu ya Awali’ wa Mei, 2020 unathibitisha changamoto ya mafunzo kwa walimu. Ndio maana @HakiElimu kwa pamoja na Chuo Kikuu Kishiriki cha @MUCE_yetu na Chuo Kikuu cha VIA tulibuni mafunzo haya"…Dkt John Kalage
#MwanzoMzuri
officialmuce retweeted
"Licha ya jitihada za Serikali kupitia Wizara husika kutoa Mwongozo wa mafunzo kazini kwa Walimu, sio Walimu wote huwa wakipata nafasi ya kujiendeleza kazini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti na Elimu ya awali ndiyo inaathiriwa zaidi’...Dkt. John Kalage.
officialmuce retweeted
‘Mafunzo kazini ni sehemu muhimu sana katika kuwawezesha na kuongeza weledi wa walimu kitaaluma na ki-vitendo, na hivyo kuchochea zaidi uwezekano wa kuboresha matokeo ya kujifunza ya wanafunzi’ ...Dkt John Kalage – Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu.
#MwanzoMzuri
officialmuce retweeted
"Shule za awali hazina michezo. Mtoto hawi mchangamfu kama hana michezo, lazima tuhakikishe tunatoa "exemption" kwenye vifaa vya michezo au viwanda vyetu vitengeneze vifaa vya michezo na tufanye jitihada kuboresha mazingira ya michezo"... DC-Iringa @Kasesela
#MwanzoMzuri
#Mkwawa
officialmuce retweeted
"Changamoto za Elimu sio lazima waseme @HakiElimu kwa sababu wanaonekana ni wanaharakati, na sisi Serikali tuziseme kwani ukikiri makosa inasaidia kujirekebisha"...Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
officialmuce retweeted
Leo Januari 9, Walimu 40 wa elimu ya awali kutoka wilaya za Iramba, Mpwapwa na Kilosa waliokutanishwa Iringa katika mfululizo wa mafunzo mahsusi ya kuwaboreshea ufundishaji kwa watoto, wanahitimu mafunzo yao yaliyoandaliwa kupitia programu ya #Mwanzomzuri.
officialmuce retweeted
Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa ndiye mwakilishi wa Serikali Katika mahafali ya Walimu wa awali waliohitimu mafunzo maalumu ya kuboreshewa uwezo, na anamuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo.
officialmuce retweeted
'Shule zinazofanya vibaya sio kosa sana la walimu ila ni kosa la mazingira, mimi nasikia wivu kwa sababu walimu wote hawa hakuna walitokea Iringa,natamani hata tufanye ushawishi kama 10 hivi wabaki hapa’...maneno ya Mkuu wa Wilaya Iringa-Richard Kasesela.
#Mkwawa.
#MwanzoMzuri
officialmuce retweeted
'Mimi ni mdau wa Elimu ya awali sana,Tanzania tuna changamoto kubwa kwenye mfumo mzima wa elimu ya awali, naomba Kamishna unifikishie Salamu. Taifa letu haliwezi kuendelea bila kuendeleza Elimu ya awali'...Mkuu wa Wilaya Iringa - Richard Kasesela.
#MwanzoMzuri














