TPDC 2026 || #TPDCMarathon2026
Bonyeza *152*00#, kisha chagua namba 4, kisha chagua namba 8, kisha chagua namba 2 ili uweze kujisajili na TPDC Marathon 2026.
"Hatua yako, Moyo wake, Okoa Maisha"
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #Shimmuta2026
.
Timu ya mpira wa miguu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza kwa kishindo mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma Taasisi na Makampuni binafsi Tanzania (SHIMMUTA 2026) yanayofanyika Mkoani Morogoro baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Memorial Academy) katika mchezo wake wa ufunguzi.
.
Ushindi huo unaipa TPDC mwanzo mzuri wa mashindano hayo, huku wachezaji wakionesha ari, juhudi na mshikamano katika kuwania matokeo mazuri.
.
Matokeo hayo ni chachu kwa Timu ya Michezo ya TPDC kwa ujumla kuendelea kupambana katika michezo inayofuata, ikiwa na dhamira ya kufanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya Shirika katika mashindano ya SHIMMUTA 2026.
.
Aidha, TPDC inashiriki mashindano haya kupitia michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa wavu kwa wanawake na wanaume pamoja na mchezo wa kuvuta kamba.
.
TPDC itakuwa tena uwanjani kesho Novemba 7, 2026 ikivaana na timu ya Shirika la viwango (TBS) katika mchezo wa mpira wa miguu kundi G.
.
#TPDCTunaboreshaMaishaNaKuwezeshaMaendeleo
1
142
Tanzania Petroleum Development Corporation retweeted
TPDC 2026 || #HaflaUtiajiSaini
.
Moja ya Nukuu muhimu kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dkt. James Mataragio.
.
Kauli hiyo ameitoa katika Hafla ya Utiaji Saini wa Leseni za Utafutaji wa Mafuta na Gesi vitalu vya Mnazi Bay North, West Songosongo, Eyasi Wembere na Lindi - Mtwara iliyofanyika jana Oktoba 28, 2026 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).
#TPDCTunaboreshaMaishaNaKuwezeshaMaendeleo
TPDC 2026 || #HaflaUtiajiSaini
.
Moja ya Nukuu muhimu kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dkt. James Mataragio.
.
Kauli hiyo ameitoa katika Hafla ya Utiaji Saini wa Leseni za Utafutaji wa Mafuta na Gesi vitalu vya Mnazi Bay North, West Songosongo, Eyasi Wembere na Lindi - Mtwara iliyofanyika jana Oktoba 28, 2026 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).
#TPDCTunaboreshaMaishaNaKuwezeshaMaendeleo
TPDC 2026 || #HaflaUtiajiSaini
.
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limepiga hatua muhimu katika kuimarisha uwezo wa Taifa wa kutafuta rasilimali za mafuta na gesi asilia, kufuatia utiaji saini wa leseni za utafutaji katika vitalu vya Mnazi Bay North, West Songo Songo, Eyasi-Wembere na Lindi-Mtwara. Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNCC), jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi.
.
Hatua hiyo inaweka msingi wa TPDC kuendeleza shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia katika maeneo hayo, kwa kutumia uwezo wake wa kitaalamu na kufanya kazi kwa kujitegemea au kwa kushirikiana na wawekezaji wenye uwezo wa kifedha na kiteknolojia. Maendeleo haya yanaendana na jukumu la Shirika la kuendeleza rasilimali za petroli nchini na kuimarisha usalama wa nishati kwa manufaa ya Taifa.
.
Utafiti katika vitalu hivyo unatarajiwa kuongeza uelewa wa uwepo na ukubwa wa rasilimali za mafuta na gesi asilia nchini, na hivyo kufungua fursa za uwekezaji katika hatua zinazofuata za uendelezaji wa rasilimali hizo. Kwa upande wa TPDC, kuimarika kwa uwezo wa kufanya tafiti kutaleta fursa ya kuongeza ushiriki wa Taifa katika hatua za awali za mnyororo wa thamani wa sekta ya petroli, huku kukiwa na uwezekano wa kuongeza upatikanaji wa nishati, ajira na shughuli za kiuchumi endapo rasilimali zitagunduliwa na kuendelezwa kibiashara.
.
Kupitia hatua hii, TPDC inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuendeleza rasilimali za mafuta na gesi asilia kwa maslahi ya Watanzania, sambamba na juhudi za Serikali za kuimarisha usalama wa nishati na kujenga msingi wa maendeleo endelevu ya kiuchumi.
.
#TPDCTunaboreshaMaishaNaKuwezeshaMaendeleo
TPDC 2026 || #HaflaUtiajiSaini
.
Viongozi, wadau wa sekta mbalimbali na wananchi wakiwasili katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) uliopo jijini Dar es Salaam kushiriki kwenye hafla ya utiaji saini leseni za utafutaji wa mafuta na gesi vitalu vya Mnazi Bay North, West Songosongo, Eyasi Wembere na Lindi - Mtwara.
.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius John Ndejembi.
.
#TPDCTunaboreshaMaishaNaKuwezeshaMaendeleo
TPDC 2026 || #UtiajiSaini
.
Wakati wa kushuhudia tukio kubwa umewadia.
.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #UtiajiSaini
Zimebaki siku 2 kuelekea tukio kubwa linalotarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #Nukuu
Moja ya nukuu kutoka kwa Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana Oktoba 18, 2026 kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #MiradiYaMaendeleo
Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) inaendelea kutekeleza miradi ya utafutaji na uendelezaji wa rasilimali za mafuta na gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa gesi na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, amesema TPDC imeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ya utafutaji na uendelezaji wa rasilimali za mafuta na gesi asilia katika vitalu vya Eyasi-Wembere, Lindi-Mtwara, Songo Songo Magharibi, Ntorya na Mnazi Bay Kaskazini.
Dkt. Homera amesema uchukuaji wa data za mitetemo katika vitalu vya Eyasi-Wembere na Lindi-Mtwara unatarajiwa kukamilika Desemba 2026.
Akizungumzia maendeleo ya kitalu cha Mnazi Bay, Mhe. Dkt Homera amesema uchimbaji wa visima vitatu, viwili vya uendelezaji na kimoja cha utafiti, umekamilika kwa mafanikio na kuongeza kiasi cha gesi inayozalishwa nchini.
Aidha, Mhe. Dkt Homera amesema wiki ijayo pia kunatarajiwa kufanyika hafla ya kusaini na kukabidhi leseni za utafiti wa mafuta na gesi kwa TPDC, itakayoshuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hatua hizi zinaonesha kuendelea kwa juhudi za Serikali kupitia TPDC katika kuendeleza rasilimali za mafuta na gesi asilia nchini kwa manufaa ya wananchi na uchumi wa Taifa.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #NyerereDay
.
Leo Oktoba 14, 2026 Taifa la Tanzania linakumbuka kifo cha Muasisi wa Tanzania na Mpigania Uhuru, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #HudumaKwaWateja
.
Tunawatakia heri ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka 2026. Mteja ni Msingi wa Mafanikio yetu, Huduma Bora ya na Viwango vya Juu ni haki yako.
.
Ahsante Mteja wetu kwa kutuamini.
Tutaendelea kukupa Huduma bora kwa viwango vya kimataifa.
.
#TunawezeshaMaisha
1
1
92
TPDC 2026 || #MaoneshoYaMadini
.
ASANTE SANA, HADI WAKATI MWINGINE TENA.
.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026|| #TaarifaKwaUmma
.
TAARIFA KWA UMMA.
.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #Pongezi
TPDC tunakupongeza Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #TPDCMarathon2026
Jisajili sasa na TPDC Marathon ili tuweze kushirikiana kwa pamoja kuokoa maisha ya mtoto.
"Hatua yako - Okoa Maisha"
#TunawezeshaMaisha
4
138
TPDC 2026 || #MaoneshoYaMadini
Karibu utembelee banda la TPDC katika Maonesho ya Tisa Kitaifa ya Teknolojia ya Madini 2026 yanayofanyika kwenye viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani Geita.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #MaoneshoYaMadini
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linaendelea kutoa elimu ya mafuta na gesi asilia kwa wananchi katika Maonesho ya Tisa Kitaifa ya Teknolojia ya Madini 2026 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani Geita.
Kupitia banda la TPDC, wananchi kutoka maeneo mbalimbali wanapatiwa elimu ya mchakato wa utafutaji, upatikanaji, uchakataji na matumizi ya gesi asilia na mafuta kwa mustakabali wa taifa.
Aidha, TPDC inatumia jukwaa la maonesho haya yaliyobeba kauli mbiu, 'Madini ni utajiri Tuwajibike kwa pamoja kufikia Dira ya Taifa 2050', kujibu maswali mbalimbali yanayohusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ili kuleta chachu ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Maonesho haya yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini, mafuta na gesi, huku TPDC ikiendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha rasilimali za nishati zinachangia moja kwa moja katika ustawi wa kiuchumi wa Watanzania na kufikia malengo ya maendeleo ya taifa.
#TunawezeshaMaisha
3
134
TPDC 2026 || #MaoneshoYaMadini
HABARI PICHA
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo katika Maonesho ya Tisa Kitaifa ya Teknolojia ya Madini 2026 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani Geita.
#TunawezeshaMaisha
TPDC 2026 || #MaoneshoYaMadini
Tunakukaribisha utembelee banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini kwa mwaka 2026 yanayofanyika kwenye viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani Geita kuanzia Septemba 23 hadi Oktoba 3, 2026.
#TunawezeshaMaisha

























