
Generally talk a lot about #M4C #KatibaMpya #ManchesterCity #HumanRights #ChangeTanzania ๐ A Business man- -C.E.O of Next Zone Shine Wear Group.
Nairobi
Joined April 2014
- Tweets212K
- Following1.9K
- Followers27.9K
- Likes269K
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
Mtaalam Pekee unaenda na ugonjwa WA kansa na akakupima kwa muda mrefu akagundua huna kansa akasema nimekukuta na dengue NI daktari ili anakusaidia
Kikatiba si vipaumbele cha mahakama kusaka adhabu kumpa mtu kumkomoa mahakama IPO kusaidia wananchi
Hili la @TunduALissu
Mmechemka
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
Tanzanian opposition leader Tundu Lissu has been sentenced to four years in jail after being arrested on treason charges in April.
The court instead convicted him of inciting unrest in a trial that has been widely condemned as politically motivated.
Tanzanian opposition leader jailed in โpolitically motivatedโ case
More on Aljazeera.com
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
Kama wasomi wa taifa wenye PhD zao ndio wapo hivi, hao wajinga wana hali gani?๐ค๐ค๐ค
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
โผ๏ธTUMFARIJI TUNDU LISSUโผ๏ธ
Kila anayeweza AFIKE kwenye msiba na aende kwenye mazishi ya Mzee Alute kumwakilishi Lissu
Tuseme kwa pamoja ๐๐ฝ I AM TUNDU LISSU
โMimi ni Tundu Lissuโ
Kushindwa kumzika mpendwa wako kwa kuzuiwa na mafedhuli inauma sana!
Naongea nikijua uchungu huu! Lissu, Heche na wanachadema walinifariji sana walipoenda kufariji familia yangu na kumzika Baba yangu! Sitasahau upendo huu! (Isipokuwa mnafiki dalali Lema huyu โ)
Kwa sasa kila anayeweza, kila mtanzania asimame na Lissu na familia yake katika huu msiba!
#FreeTunduLissu
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
Kama uchaguzi ulivurugwa kwa sababu ya uchochezi; mshindi alipataje 98%?
Mchochezi alivurugwa vipi na hizo asilimia (%) zilitoka wapi?
Shame on you Judiciary.
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
Baada ya hukumu ya leo; kama kuna Mtanganyika atakaethubutu kushauri au kuunga mkono MARIDHIANO atakuwa mjinga na mpumbavu wa hali ya juu.
Watawala hawataki haki wala amani wanachotaka ni kujikita madarakani kwa gharama yoyote.
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
Ujue bila ya wanaharakati kutoboa siri ya hukumu ya Lisu. Ujue Lisu alikuwa anakula miaka tano wazee. Ukute wanaharakati ndo wamesababisha wale jamaa wakapunguza mwaka mmoja alafu anakuja yule dalali wa machame anasema tuwapuuzie wanaharakati. Fuck๐ฎ
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
pole sana mzee wangu alute mahakama imekuangusha. lakini nakubaliana na wewe, lazima tuishi kwa matumaini. mapambano yaendelee. uendelee kupumzika kwa amani, na niendelee kukuweka wewe binafsi na familia yako kwenye maombi wakati wa kipindi hiki kigumu.
๐ฅ: @izzy_pro_director:
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
Tundu Lissu ahukumiwa kifungo cha miaka minne jela, je, ipi hatma ya cha... youtube.com/live/jbX8FXgftkEโฆ via @YouTube
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
ARBITRARY ARRESTS-UKAMATAJI HOLELA
Neema mhanuzi katibu wa Bawacha mkoa wa kigoma amechukuliwa na watu waliojitambulisha kua ni Askali wa Jeshi la police.
Amechukuliwa Nyumbani eneo la Mwasenga, kata ya Buhanda. Kigoma mjini majira ya SAA 12 Jioni.
Viongozi wa chadema pamoja na familia wamemtafuta vituo vyote vya police mjini kigoma, police wamekanusha kua hawamshikilii wao, ingawa wamesema warudi kesho asubuhi kituo kikuu cha police Mnarani.
Free Neema Mhanuzi now
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
Mwaka 1957 wakoloni wazungu walimfungulia Mwalimu Nyerere kesi ya uchochezi.
Kwenye hiyo kesi wakoloni wazungu walimkuta na hatia mwalimu Nyerere. Pamoja na kumkuta na hatia Mwalimu wakoloni hawakumfunga Nyerere gerezani bali walimlipisha faini na akaenda nyumbani.
Miaka zaidi ya 70 baadae, mahakama chini ya majaji kina Ndunguru na Jaji mkuu Masaju.
Yenyewe imejiundia kosa, imejitafutia ushahidi, imemfunga kiongozi wa upinzani nchini tena kwenye kosa lenye faini.
Ccm na serikali ya Samia Suluhu Hassan ni makatili kuliko wakoloni wazungu.
Historia itawaweka mnapostahili.
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
๐ฅนDaah Huyu Jamaaa ๐ซก๐ซก๐ฉ๐๐พ
Mpaka internet inazimwa HUYU NI MWANAUME๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐๐พ
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
Kwa mnaosubiria video kutoka kwangu leo, msisubiri.
Nimeona nijipe muda, moyo wangu upoe kidogo na maumivu yaliyo rohoni mwangu yastahamilike kidogo la sivyo hakuna la maana nitakaloongea zaidi ya kuwamwagia machozi mwanzo hadi mwisho wa videoโฆ..
MMAREKANI MWEUSI ๐ฐ๐ช๐บ๐ธ retweeted
SIKU YA AIBU KWA UTAWALA WA SHERIA!
Sisi ni nchi inayofuata mfumo wa Common Law, siyo mfumo wa Civil Law Katika mfumo wetu, Mahakama ni mwamuzi huru na asiyeegemea upande wowote (impartial adjudicator), siyo mpelelezi, siyo mwendesha mashtaka, wala siyo mtunga mashtaka.
Lakini kwa hali ya kushangaza, leo tunakutana na Mahakama inayochukua majukumu yote kwa wakati mmoja: inaandaa shtaka (charge), inafanya uchunguzi, inaendesha mashtaka, inakusanya ushahidi, inabaini kosa, inamkuta mtuhumiwa na hatimaye kumhukumu, bila kumpa nafasi ya kusikilizwa ipasavyo.
Huu siyo utendaji wa Mahakama inayosimamia haki. Huu ni kuvuruga misingi ya haki asilia (Principles of Natural Justice), haki ya kusikilizwa (Right to be Heard) na kanuni ya kutokuwa hakimu katika shauri lako mwenyewe (Nemo Judex in Causa Sua).
Mahakama haiwezi kuwa mlalamikaji, mpelelezi, mwendesha mashtaka na hakimu kwa wakati mmoja.
Hata kama ni kosa dogo lazima liwe cognate offence yaani kosa linaloendana au kuhusiana na kosa analoshtakiwa. Naliwe sehemu ya shitaka na ushahidi utolewe kuhusu hilo na mtuhumiwa ajitetee.
Na pia ni Kanuni za Msingi katika Taifa letu kwamba kunapokuwa na adhabu ya Kigungo na Faini au vyote kwa pamoja ni lazima uanze kwanza na adhabu ya faini akishindwa kinafuata kifungo. HII NI AIBU KUBWA.
Kazi ya Mahakama ni kutenda haki kwa kusikiliza pande zote kwa usawa, siyo kutafuta au kubuni njia za kumtia mtu hatiani.
Tunapofika hapa, tunakuwa hatujadili tena hatima ya mtuhumiwa mmoja tu; tunajadili uhai wa utawala wa sheria katika nchi yetu.
UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI NDIVYO VITALIPONYA TAIFA!
BAK MWABUKUSI



















