TzConnect retweeted
Wanafunzi wanane waliohitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Aboud Jumbe iliyopo Kata ya Mji Mwema Wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam wamewaomba radhi Wazazi, Walezi, Walimu, Wadau wa Elimu, Viongozi na Watanzania kufuatia picha mjongeo iliyosambaa mitandaoni ikiwaonesha wakitoa lugha zisizofaa.
Wanafunzi hao wameomba msamaha huo leo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dalmia Mikaya ambaye ameitisha kikao katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni kikiwahusisha Wanafunzi hao, Wazazi/Walezi na Maafisa mbalimbali wa Serikali.
Wanafunzi hao wamesema ni shetani tu aliwapitia na furaha ya kuhitimu masomo iliwazidi hadi kujikuta wanafanya matendo yasiyofaa na wameahidi hawatorudia tena.
Kwa upande wake Mikaya amewasihi Wazazi, Walezi na Walimu kuungana pamoja katika kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya Watoto wawapo shule na majumbani ili kudhibiti vitendo vya hovyo huku akiwapiga marufuku Wanafunzi hao kutorudia kufanya mambo kama hayo na kwamba wamesamehewa na hawatapewa adhabu yoyote.
#MillardAyoUPDATES
TzConnect retweeted
PROACTIVE PLANNING
Proactive planning is the cornerstone of effective national food security, especially when facing unpredictable weather patterns like a forecast El Niño. By securing maize seed and top-dressing fertiliser well ahead of the summer season, the Government is eliminating traditional delays and ensuring that farmers are equipped for success before the rains arrive. With about 45 percent of required basal fertiliser already distributed and millions of plots prepared across the country, the Second Republic is translating policy commitments into tangible, ground level support. Early availability of inputs empowers smallholder farmers to plant on time, optimize their yields, and maintain consistent food production regardless of external climatic pressures.
#NyikaInovakwaNeveneVayo #EDtheGameChanger #NDS2
TzConnect retweeted
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limemshikilia Verediana Levee, mfanyakazi wa ndani, kuhusiana na kifo cha mtoto William Mathayo (miaka 5).
Mtoto alipatikana amefariki ndani ya nyumba yao, Mtaa wa Ibolelo, Kata ya Nyankumbu, Wilaya ya Geita. Tukio lilitokea Oktoba 24, 2026, majira ya saa 4:00 asubuhi, wakati mtoto akiwa amelala kitandani.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, mtuhumiwa anadaiwa kumwagia kitu kisha kumkaba shingo. Wazazi hawakuwepo nyumbani wakati tukio linatokea. Chanzo cha tukio hilo kinaaminika kuwa imani za kishirikina.
Polisi wanasema uchunguzi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
#MeaMswahiliUPDATES
VIDEO:
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye, amebainisha kuwa kuridhiwa na kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) nchini ni ushahidi usiopingika kuwa Tanzania bado ni kisiwa cha amani duniani, huku akiwataka Watanzania kulinda amani na utulivu kama mtaji mkuu wa taifa.
Nape ameyasema hayo leo, Oktoba 27, 2026, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kumpongeza, kumtia moyo na kumshika mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huo mkubwa wa kimataifa nchini kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026.
Akizungumza bungeni, Nape ameeleza kuwa pamoja na maneno yote yanayoweza kusemwa, uamuzi wa dunia kuipenda na kuileta mikutano mikubwa nchini na wajumbe kuja na kuondoka salama unathibitisha kuwa Tanzania bado ni sehemu salama
"Ukiona vinaelea vimeundwa, azimio hili lina lengo la kumpongeza, kumtia moyo, kumshika mkono Rais wetu ambaye ameunda hivi ambavyo leo tunavisifia vinaelea... Ukweli kwamba Tanzania bado ni kisiwa cha amani, pamoja na maneno yote lakini sisi bado ni kisiwa cha amani ndio maana dunia iliridhia, ikaamini, ikaja Tanzania ikafanya mkutano huu mkubwa na wakaondoka salama. Hiki bado ni kisiwa cha amani, tunao wajibu wa kuendelea kukitunza kisiwa hichi cha amani", ameeleza Nape.
Nape amebainisha kuwa michango ya wabunge mbalimbali waliosema bungeni imedhihirisha kuwa amani na utulivu wa nchi si jambo la kuchukulia kawaida, bali ni mtaji mkuu ambao lazima uendelee kulindwa na kutunzwa.
TzConnect retweeted
Parliament has passed a motion to praise President Samia Suluhu Hassan for facilitating the hosting of the 153rd Assembly of the Inter-Parliamentary Union (IPU) in Arusha from October 5 to 9, 2026.
instagram.com/reel/DfB6I-xOT…
TzConnect retweeted
Story kubwa ulimwenguni ni Dogo alivyowapiga vyenga hadi watu walimaindi...
Au kwa kuwa ni ngozi nyeusi ndio maana wamemtendea vile?
Hivi wazazi wote wanafanana duniani?
Au kuna shida sehemu?
Ni Nevada mwenye umri wa miaka 3.
Sio 13. Sio 30. Ni 3 walimwengu.
Bado ni mtoto anayehitaji kusaidiwa kufunga viatu na watu wazima...
Lakini huko Winter Park, Florida, waliamini dogo ni tatizo linalohitaji kushughulikiwa.
Kwa mujibu wa familia yake, Nevada alikuwa anacheza kwenye ligi ya soka ya watoto ya i9 Sports dhidi ya watoto waliomzidi umri kwa miaka miwili.
Siku zilivyozidi kwenda, hakuna hata mmoja wa wale watoto wa miaka 5 aliyeweza kumpokonya mpira Nevada.
Baada ya walimwengu kuona kipaji cha bwana mdogo, walianza kulalamika Wakasema.
"Dogo anakaa na mpira sana, anajaribu kujionyesha, ni mpenda sifa."
Wao walitaka kutuaminisha kwamba mtoto mdogo kujionyesha akicheza soka vizuri kwenye mchezo wa soka ni kosa.
Walimwengu wakawaita polisi kwenye uwanja wa soka wa watoto...
Kwa sababu ya Nevada ambaye hakuwapigia wenzake pasi.
Ndio, pasi tu ndiyo ilikuwa tatizo kwa walimwengu, hadi kumuitia polisi mtoto mdogo kwa sababu ya kumiliki mpira kwa dakika nyingi.
Familia inasema baadaye walirudishiwa pesa yao ya usajili wa msimu.
Pole sana wazazi wa Nevada Pierre, hao ndio walimwengu. 🥶
TzConnect retweeted
Droo ya makundi CAF hadharani leo
mwananchi.co.tz/mw/michezo/s…
TzConnect retweeted
MAKE YOUR WEDNESDAY DELICIOUS!
Take a break from your busy week and enjoy our Indian, Chinese and Continental favourites in a warm and welcoming atmosphere.
Good food is always a great idea!
Wampewo Avenue, Kololo, Kampala
0751 903 647 | 0765 946 392
#Kampala #UgandanFood
TzConnect retweeted
Arsenal yatolewa na vibonde Kombe la Carabao
mwananchi.co.tz/mw/michezo/m…
TzConnect retweeted
#HABARI Serikali ya kijeshi ya Niger imeishutumu nchi jirani ya Chad kwa kutekeleza shambulizi la ndege isiyo na rubani katika ardhi yake, lililosababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine kadhaa, huku ikidai kuwa shambulizi hilo lilifanyika kwa uungwaji mkono wa Ufaransa.
Katika taarifa iliyotangazwa kupitia televisheni ya taifa, serikali hiyo imedai kuwa ndege hiyo ilirushwa kutoka eneo la Chad na kushambulia kijiji kimoja katika eneo la Agadez, kaskazini mwa Niger, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Niger imesema ina ushahidi kuhusu shambulizi hilo na imeanzisha uchunguzi, huku ikipanga kumwita balozi wa Chad nchini humo kuwasilisha malalamiko.
Serikali hiyo pia imesema inakusudia kuchukua hatua za kisheria katika mahakama za kimataifa, ikidai kuwa tukio hilo limekiuka mamlaka na uhuru wa nchi hiyo.
Hadi sasa, Chad na Ufaransa hazijatoa tamko kuhusu tuhuma hizo. Madai hayo yameibuka wakati uhusiano wa Niger na Ufaransa ukiendelea kuzorota tangu mapinduzi ya kijeshi ya Julai 2023, yaliyosababisha wanajeshi wa Ufaransa kuondoka Niger.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
TzConnect retweeted
⏳🎓 WANAFUNZI WAPYA MUHAS, JIANDAENI!
Siku za usajili zimekaribia! Jiandaeni kujiunga na MUHAS. Tunawasubiri kwa hamu kuwakaribisha!
#MUHAS #KaribuMUHAS #MUHAS2026
TzConnect retweeted
Breaking news;
President Yoweri Museveni endorsed CDF Gen Muhoozi Kainerugaba Museveni as next president at the NRM CEC meeting
TzConnect retweeted
AMANI NI MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFA LETU
Tanzania ni nyumba yetu sote. Tofauti zetu za kisiasa, kijamii na kiitikadi zisituondolee utu, umoja na upendo tuliojenga kama taifa.
Tuheshimiane, tusikilize maoni ya wengine, tutatue tofauti zetu kwa mazungumzo na tuepuke vitendo vya uchochezi na vurugu.
Tuilinde amani, tudumishe umoja na tuheshimu utu wa kila Mtanzania. Taifa letu likiwa na amani, tuna nafasi kubwa zaidi ya kujenga maisha bora kwa wote.
🇹🇿 Amani ni jukumu letu sote. Tanzania kwanza!
#AmaniYaTanzania #TanzaniaYetu #UmojaNiNguvu
TzConnect retweeted
Mtoto Mpendwa Wa Hayati Rais Benjamin Mkapa, Baba Yake Alipenda kumuita Nico. Walizaliwa Wawili tu Yeye Nico na nduguye Stephano Mkapa, Ukipenda Muite "Steve." Hawa Ndio Watoto Wawili Wa kiume Wa Hayati Rais Mkapa.
Miaka Kumi ya utawala Wa baba Yake Kama Rais Wa awamu ya Tatu (1995-2005) Nico Alikuwa masomoni Nje ya Nchi na ndio Maana Kuna watu mpaka Leo wapo walioamini Kuwa Hayati Mzee Mkapa Hakuwa Na Watoto.
Nico Ni mbobezi Wa Sayansi ya siasa na historia (Political Science and History) aliyosomea Chuo Kikuu Cha Carleton (1997-2000), Alikaa mwaka Mmoja tu Kisha Mwaka (2002-2005) Alijiunga na Chuo Kikuu Cha Lancaster, Uingereza Kusomea Sheria (Bachelor of laws) hii ikiwa ni shahada Yake ya pili na alimaliza masomo mwaka Ambao baba Yake Alikuwa anamalizia kipindi Chake Cha pili Cha urais.
Na hivi karibuni ameongeza elimu Katika masuala ya utawala, Post Graduate Diploma in Leadership aliyoipata Taasisi ya Uongozi na Aalto EE (2022 – 2023).
kwasasa Bw. Nicholaus Mkapa ni Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Kabla ya nafasi aliyonayo Amewahi kutumikia nafasi kadhaa Serikalini Kama ifuatavyo,
Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (Aprili 2024 – Hadi sasa)
Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo (Februari 2023 – Machi 2024)
Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Septemba 2019 – Februari 2023)
Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Oktoba 2017 – Septemba 2019)
Wakili wa Serikali Mwandamizi – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Januari 2007 – Oktoba 2017).
Hayati Rais Magufuli Ndiye aliyemtoa kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu Wa Serikali Akiwa wakili mwandamizi Wa Serikali na kumpeleka Wizara ya habari na utamaduni, Sanaa na michezo mwaka 2017 Kama Naibu Katibu Mkuu, Tangu hapo amekuwa Akihudumu nafasi Hiyo Wizara mbalimbali.
Huyu Ndiye Nico Mtoto Mpendwa Wa Uncle Ben.
TzConnect retweeted
President Yoweri Museveni has prioritised access to modern farm equipment, supporting the transition from traditional to more productive agricultural systems.
TzConnect retweeted
🚨𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄
Kulingana na hesabu ya karibu asilimia 50 ya kura, muungano wa Benjamin Netanyahu una viti 55, muungano wa Gadi Eisenkot una viti 50, na vyama vya Waarabu vina viti 15.
Hakuna upande uliopata viti 61 vinavyohitajika kuunda serikali katika Bunge la Knesset lenye viti 120. Matokeo haya bado si ya mwisho; hesabu inaendelea na kura za “double envelopes” (ikiwemo za wanajeshi) zitahesabiwa baadaye.
#MeaMswahiliUPDATES
TzConnect retweeted
🇨🇩 Rais wa DRC amewasili Moscow kushiriki Mkutano wa Tatu kati ya Urusi na Afrika.
Félix Tshisekedi anatarajiwa kufanya mazungumzo na Vladimir Putin katika ikulu ya Kremlin.
✍️📄 Mikataba mitatu ya ushirikiano imepangwa kusainiwa, ikiwemo mafunzo ya ufundi kwa vijana wa Kongo kupitia mpango wa "Alabuga Start", ofisi ya Rais imeripoti.






































