Pinned Tweet
Mithali 9:11
Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa. Amina 🙏
Happy Birthday 🎂 To Me 🙏
Necto Kitiga retweeted
uhalifu na uonevu serikali inafanyia w’nchi utakuja kuliangamiza hili taifa. kama ilivyo kwa mtu, taifa nalo lina roho, ‘a soul.’ serikali is tearing that up, kila siku. hata kuwatafuta waathirika wa ukatili wake wenyewe na kuwasaidia imeshindwa? sawa:
Necto Kitiga retweeted
Appreciation post kwa Baraza la Maaskofu wa Katoliki jana walijua kututendea Haki Watanzania, Mungu awabariki sana.🙏
Necto Kitiga retweeted
BAVICHA iko imara. Ushawishi mkubwa kwa Wenyeviti wa Kanda 3 & Mikoa 11 tunaufuatilia kwa makini na safari zinazoandaliwa. Tutawatahadharisha kuhusu hizo Biashara haramu. Udalali hautaruhusiwa miongoni mwetu Vijana. BAVICHA sio kichaka cha kuhubiri Maridhiano ya Ulaghai.
Necto Kitiga retweeted
Hon. Pam Cox MP raises Tundu Lissu’s case in the @UKParliament. Charged with treason for calling for electoral reform, he faces a possible death sentence. The UK remains “gravely concerned.”
This builds on US @StateDept concerns and bipartisan Senate bill S.4577 (@SenatorShaheen & @tedcruz). With the 6 November verdict approaching, the UK Parliament must work with the US Congress and State Department to protect democracy, human rights, and the rule of law in Tanzania.
#FreeTunduLissu
Necto Kitiga retweeted
TAARIFA KWA UMMA.
@ChademaTZ2 @HecheJohn @AdvMahinyila @NectoKitiga @duahamud @RevlineMbugi @FeliusFesto
Necto Kitiga retweeted
CHADEMA is deeply grateful to Hon. Pam Cox, Member of the UK Parliament, for expressing her grave concern over the politically motivated and fabricated treason charges against our party chairman, Hon.Tundu Lissu. If convicted on 6 November, he could face death penalty.
We also take note of the @UN Working Group’s opinion, which found his detention to be arbitrary, unlawful and without sufficient legal basis.
This is a significant affirmation of the serious concerns we have consistently raised regarding the violation of his fundamental rights.
We appreciate Hon. Pam Cox’s and the British High commissions solidarity and continued international attention. However, more engagement and intervention are needed to ensure that justice is served and that Tanzania remains committed to democratic principles, respect for human rights and the rule of law.
Ultimately, a democratic Tanzania governed by the rule of law is in everyone’s interest.
Necto Kitiga retweeted
Tundu Lissu was charged with (politically motivated) Treason after calling for electoral reform.
The sentence for Treason in Tanzania is nothing else other than DEATH.
The world is waiting for November 06
Thanks Hon Pam Cox for raising this matter in the House Of Commons
Necto Kitiga retweeted
Mzee wa Atikali (Ganga Benard Mlaponi) leo 30.10.2026 huko facebook ameandika kuwa iwapo bado, WANASHERIA NCHINI WATAKUWA WAMESHINDWA KUMPATA MWANASHERIA MAHIRI KUTEKELEZA AGIZO LA MHE RAIS SAMIA la
Julai 13, 2026 huko A-Town kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali, ambapo akiwa mgeni rasmi alikataa pendekezo lao la kuita kituo cha Umahiri wa Sheria (Center of Excellence) jina lake. Akawaagiza atafutwe Mwanasheria Mahiri nchini ili Kituo cha Umahiri cha Sheria (Center of Excellence) kipewe jina la Mwanasheria huyo. Ikiwa kweli utekelezaji wa agizo hilo bado, Mzee wa Atikali amependekeza kituo hicho kipewe jina la Hayati Mark Bomani na kiitwe _"Mark Bomani Center of Excellence" Ametoa sababu kadhaa, kubwa ni kwamba ndiye alikuwa "Solicitor General" wa kwanza nchini Mwafrika na mwaka 1965 aliteuliwa kuwa "Attorney General" wa kwanza nchini Mwafrika akiwa kijana mdogo tu wa miaka 32. Aliacha kazi hiyo ya AG mwaka 1976.
Mark Bomani alipewa jukumu kubwa na Rais Nyerere la kutafuta Majaji na Mahakimu kwani wakati huo Taifa letu lilikuwa ni Taifa changa ambalo wananchi wachache sana ndio walikuwa na elimu ya Sheria hivyo ukawepo uhaba mkubwa wa Majaji na Mahakimu.
Atikali imeeleza jinsi Mark Bomani alivyosafiri hadi nchi za Africa magharibi (Nigeria na Ghana) na visiwa vya Caribbean (Trinidad & Tobago) alikomuibua Phillip Telford Georges aliyekuja kuteuliwa na kuapishwa na *Rais Nyerere* kuwa Jaji Mkuu 1965. Mchango wa Mark Bomani kwenye sekta ya Sheria hauna mfanowe.
Tumeelimishwa hii haitakuwa mara ya kwanza kwa "Center" kupewa jina la AG ili kuenzi mchango wake: Kituo cha Robert Kennedy Human Rights Centre kinabeba jina la aliyekuwa AG wa 64 wa USA kuenzi mchango wake. Kituo cha Janeth Reno Center for Youth Justice kinamuenzi Mama aliyekuwa AG wa 78 nchini USA na Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo kuenzi mchango wake baada ya kuteuliwa na Rais Bill Clinton 1993 na kuthibishwa na Seneti.
Mimi ninaunga mkono hoja ya Mzee wa Atikali na hapohapo kusisitiza na kukumbushia pendekezo langu kuwa huko Dodoma jina la Sir George Clement Kahama lisisahaulike. Aidha huko Muhimbili Profesa Phillemon Sarungi apewe taasisi kamili, MOI iwe SOI. Tulielezwa alipewa wodi. Nashukuru hatua hiyo lakini mimi naamini haitoshi tunaweza kumuongezea bila madhara yoyote.
Necto Kitiga retweeted
mara ya mwisho mahakama yetu kuombwa itoe agizo kama hili iligoma, ikisema eti waombaji hawakuthibitisha kwamba polisi wanamshikilia aliyetekwa. mahakama, kwa makusudi, ilijisahaulisha kwamba ni wajibu wa polisi kuhakikisha usalama wa raia, haijalishi ni wao wameteka au la:
Necto Kitiga retweeted
Kesi imefunguliwa wiki hii
Imepangiwa Jaji Wiki hii
Imesikilizwa pande zote mbili wiki hii
Uamuzi umetoka wiki hii
Utekelezaji unapaswa kuanza wiki hii
Mkiambiwa wenzenu wamewazidi mnaanza kulalamika!
Mahakama zenu zinaweza kutoa haki kwa wakati?
#FreeTwahaMwaipaya
Necto Kitiga retweeted
Ghasia za Uchaguzi Tanzania: Mwaka mmoja baadaye, familia bado zinatafuta haki
bbc.in/4iJATA2
Necto Kitiga retweeted
Leo ni siku ya sita bado hatujui Twaha Mwaipaya kapelekwa wapi, tkumpazia sauti huenda sauti zetu zikasaidia.
#FreeTwahaMwaipaya
“Mungu atuhurumie,lakini kama kuna wengine waliofanya makosa ambao wanashikiliwa kwasababu za siasa hawapaswi kuuwawa” Askofu Wolfang Pisa.
Necto Kitiga retweeted
Ndugu yangu Twaha Mwaipaya BADO hatujampata.
Tuendelee kuweka #FreeTwahaMwaipaya au kurepost bila kuchoka kama ambavyo alikuwa mtu asiechoka juu ya kupambania nchi yake.
#FreeTwahaMwaipaya
REPOST 200
Necto Kitiga retweeted
Roho za wote waliouawa katika zile siku tano za majonzi, kuanzia tarehe 29 Oktoba 2025 zipumzike kwa amani ya milele.
Bwana azifariji familia zinazoomboleza, hasa zile ambazo bado zinawatafuta wapendwa wao waliopotea. Awaponye waliojeruhiwa na kuwaimarisha wote wanaoendelea kubeba uchungu wa siku zile za maafa.
Ee Bwana, uwajalie pumziko la milele, na mwanga wa milele uwaangazie. Wapumzike kwa amani. Amina.
Necto Kitiga retweeted
Siku kama ya leo tarehe 29 Oktoba 2025 kuanzia majira ya saa tano asubuhi,maandamano ya kuikataa @ccm_tanzania na Mwenyekiti wake yalianza.Maandamano hayo yalifanyika kwa kuwa wananchi walijiridhisha kwamba maoni yao yakudai mabadiliko ya kiuchaguzi na katiba Mpya hayasikiliswi kwa njia za kawaida.
Maelfu ya wananchi walitoka majumbani mwao kwa wingi wao na kuonesha hali ya kumkataa Samia waziwazi.Waliimba “Samia Must Go” na “hatumtaki Samia” kwa sauti kubwa huku wakitembea kuelekea Ikulu,wakionesha azma yao ya kudai haki,mabadiliko na utawala bora.
Kiichofuata ni ukurasa wa giza kwenye hiatoria ya nchi yetu.
Kwa hofu ya nguvu ya umma na uwezekano wa wananchi kufanikiwa kuonesha wazi kukataa kwao uongozi uliopita, vyombo vya dola viliingia barabarani. Maandamano yakageuka kuwa maafa makubwa, yaliyosababisha vifo vya Watanzania wengi katika kile kinachokumbukwa leo kama mauaji ya Oktoba 29, 2025 (29th October Massacre).
Hofu ya dola kwa nguvu ya wananchi ikageuka kuwa maumivu kwa taifa zima. Serikali ikazima intaneti, mawasiliano yakakatika na familia nyingi zikakosa taarifa za wapendwa wao. Wazazi wakawapoteza watoto wao, wanawake wakabaki wajane na watoto wakabaki yatima. Familia nyingi zikaachwa na majeraha ambayo hayatafutika kirahisi.
Baada ya hapo bado watawala wakamuapisha mtu wao,na sasa nchi inatawaliwa na Serikali haramu isiyotakiwa na wananchi wake.
Tanzania imekuwa nchi ya kidikteta/kiimla ambayo haifuati utawala wa sheria wala kudhamini haki za binadamu.Utekaji,mauaji na kesi za kubambikiana zimekuwa jambo la kawaida.Mamlaka zinazo husika zinatazama na kukaa kimya,kwa kuogopa kuvuliwa nyadhifa zao.
Mpaka nani afe ndio mambo ya badilike?Je watakao kufa kwenye nchi hii ni Chadema peke yao kwa kudai haki,uwajibikaji,na utawala bora?
Damu za Watanzania haziwezi kamwe kumwagika bure,na mambo yakaendelea kuwa business as usual.
IT IS IMPOSSIBLE
Leo, tarehe 29 Oktoba 2026 tunawakumbuka na kuwaombea wote waliopoteza maisha yao katika matukio ya Oktoba 29, 2025. Tunazikumbuka familia zilizopoteza wapendwa wao, manusura wanaoendelea kuishi na majeraha ya kimwili na kisaikolojia, pamoja na Watanzania wote walioathiriwa na mauaji hayo.
Tunawaahidi kwamba kumbukumbu zao zitaendelea kuwa sehemu ya mapambano yetu ya kudai taifa lenye haki, uhuru, demokrasia na utawala bora.
HATUTASAHAU NA HATUWEZI KUNYAMAZA.
#Freedomiscomingtomorrow
#Hatutasahau
#FreeTunduLissu
#FreeJohnPambalu
#FreeTwahaMwaipaya
#KatibaMpyaNiSasa
#VivaChademaViva.
Necto Kitiga retweeted
Today, the U.S. Embassy community joined me to honor the memory of all those who lost their lives in the violence surrounding Tanzania’s October 2025 general elections. We remember them, and the families who still grieve and seek answers. As I said to the U.S. Senate during my confirmation hearing, this will not be swept under the rug.
VIDEO:
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) @THRDCOALITION , Wakili Onesmo Olengurumwa @OlengurumwaO amesisitiza kuwa taifa linapaswa kutibu majeraha, kuwajibika, na kukaa mezani kutafuta ukweli kuhusu matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, badala ya kusahau yaliyotokea.
Wakili Olengurumwa ameyasema hayo leo, Oktoba 29, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa Ibada maalum ya kuwakumbuka waliopoteza maisha, waliopotea, na majeruhi wa matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.
Akimulika haja ya kukabiliana na ukweli badala ya kupuuza changamoto zilizojitokeza, Wakili Olengurumwa amerejea methali za Kiswahili akionya kuwa kuweka kichwa chini kama mbuni hakutatui matatizo ya nchi.
“Waswahili wanasema taifa lisilokumbuka misiba yake ni taifa lisilokumbuka furaha zake. Maana yake tukijidanganya kana kwamba hatukupata msiba maana yake tunakuwa tuko tayari kuendelea kuwa katika eh changamoto... Sisi kama taifa hatupaswi kufikiri kwamba kwa kuweka kichwa chini kama anavyofanya mbuni basi kila kitu kinakuwa salama”, ameeleza Olengurumwa.
Olengurumwa amebainisha kuwa vitabu vitakatifu vya dini zote mbili za Uislamu na Ukristo kwa maana ya Qurani na Biblia vinafundisha kuwa haki, rehema, msamaha, amani, na ulinzi wa uhai ndio msingi mkuu wa jamii yenye mshikamano. Ameeleza kuwa Qurani inasisitiza kujibu uovu kwa namna iliyo bora zaidi ili uhasama ubadilishwe kuwa ukaribu, huku vitabu vya Kikristo vikihimiza kuondoa uchungu na hasira na badala yake kujenga huruma na msamaha.































